Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Costa ageuka lulu, Man United, Arsenal za muwinda

Muktasari:

  • Inaelezwa timu nyingine kadhaa zinaweza kuongezeka kadri siku zinavyosogea, huku mchezaji huyo akidaiwa kuwaeleza watu wake wa karibu kwamba anakusudia kuieleza Porto imuache aende akatafute changamoto katika vikosi vingine Ulaya, baada ya kuona kwamba soko lake limezidi kupaa.

MANCHESTER United na Arsenal zote zinaendelea kumfuatilia kwa karibu beki wa kulia wa Porto, Alberto Costa, mwenye umri wa miaka 22, lakini zinakabiliwa na ushindani kutoka Paris Saint-Germain ambayo pia imeonyesha kuhitaji huduma yake katika dirisha dogo la Januari, mwakani.

Inaelezwa timu nyingine kadhaa zinaweza kuongezeka kadri siku zinavyosogea, huku mchezaji huyo akidaiwa kuwaeleza watu wake wa karibu kwamba anakusudia kuieleza Porto imuache aende akatafute changamoto katika vikosi vingine Ulaya, baada ya kuona kwamba soko lake limezidi kupaa.

Hata hivyo, Porto inadaiwa kwamba haipo tayari kumwachia kuondoka katika dirisha dogo kwa sababu inakabiliwa na mashindano mengi yakiwamo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwamba, itasikiliza ofa zitakazofikishwa mezani baada ya msimu huu kumalizika.

Mchezaji huyo amegeuka kuwa beki anayetazamwa sana kwa sasa kutokana na namna anavyocheza soka la nguvu, akili na kiwango cha juu ya maamuzi jambo ambalo limeifanya timu yake kutopoteza mechi hadi sasa katika Ligi kuu Ureno (Primera Liga) msimu huu.


Raheem Sterling

WINGA wa zamani wa Chelsea, Liverpool na Manchester City, Raheem Sterling, amepewa ofa na klabu mbili za Ligue 1 nchini Ufaransa, lakini zote awali hazikuvutiwa na huduma ya Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye kwa sasa hana klabu.


Abdelhamid

NEWCASTLE United inaendelea kumfuatilia kwa karibu beki wa Rennes na timu ya taifa ya Morocco, Abdelhamid Ait Boudlal, mwenye umri wa miaka 20, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka Everton, Brentford na Hull amabzo pia zinadaiwa kuulizia upatikanaji wake katika dirisha dogo la Januari.


Ibrahim Maza

ARSENAL na Tottenham Hotspur zinaendelea kumfuatilia kiungo wa kimataifa wa Algeria anayecheza Bayer Leverkusen, Ibrahim Maza, mwenye umri wa miaka 20. Maza amekuwa akipambania namba katika kikosi cha Leverkusen, lakini ni mara chache anacheza kwa sasa.


Joe Willock

RAIS wa Besiktas ya Uturuki, Serdal Adali, ameahidi kumsajili Joe Willock, mwenye umri wa miaka 27, kutoka Newcastle United mwezi Januari, akidai kwamba kiungo huyo Mwingereza tayari ameshachagua makazi yake mapya nchini Uturuki.  Besiktas inapambana kuweka mambo sawa katika Ligi Kuu Uturuki kwa sasa.


Joao Felix

MSHAMBULIAJI wa Al-Nassr na timu ya taifa ya Ureno, Joao Felix, ana nia ya kurejea kucheza soka barani Ulaya, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 hajazungumzi klabu anayoweza kujiunga nayo. Hata hivyo, kuna taarifa kwamba timu kadhaa za Hispania zinamhitaji Januari, mwakani.


Tyrick Mitchell

CHELSEA inamfuatilia beki wa kushoto wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Tyrick Mitchell, mwenye umri wa miaka 27, lakini huenda ikakabiliwa na ushindani kutoka Manchester United na Liverpool ambazo pia huenda zikagonga hodi katika dirisha lijalo kutokana na kuvutia naye.


Tchouameni

LIVERPOOL bado inamtaka kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Aurelien Tchouameni, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo ya La Liga wakati wa kiangazi. Tchouameni pia alikuwa akitakiwa na Manchester United kabla ya kuachana naye.


Erling Haaland

MANCHESTER City inadaiwa kuweka bei kubwa kwa ajili ya mshambuliaji wa kimataifa wa Norway, Erling Haaland, 26, iwapo timu hiyo itashushwa daraja kutoka Ligi Kuu England kutokana na kukiuka kanuni za kifedha. Taarifa mbalimbali za usajili Ulaya zimeanza kumhusisha kuondoka City iwapo itashushwa daraja.


Ethan Ampadu

LEEDS United haina mpango wa kumuuza beki wa kimataifa wa Wales, Ethan Ampadu, mwenye umri wa miaka 26, licha ya kuhusishwa na kurejea katika klabu yake ya zamani, Chelsea. Mchezaji huyo amekuwa katika kiwango bora tangu alipoondoka Chelsea na hivyo kuzifanya timu nyingi kuanza kummezea mate.