Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yafikia patamu kwa Jamie Gittens

Muktasari:

  • Inaelezwa Chelsea imeshafikia hadi makubaliano binafsi na Gittens mwenyewe na sasa inazungumza na Dortmund ambayo imesisitiza kuwa inahitaji Pauni 50 milioni ili kumuuza staa huyo.

CHELSEA iko karibu kukamilisha dili la kumsajili winga wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya vijana ya England chini ya miaka 21, Jamie Gittens, mwenye umri wa miaka 20, katika dirisha hili.

Inaelezwa Chelsea imeshafikia hadi makubaliano binafsi na Gittens mwenyewe na sasa inazungumza na Dortmund ambayo imesisitiza kuwa inahitaji Pauni 50 milioni ili kumuuza staa huyo.

Mabosi wa Chelsea wanajaribu kufanya mazungumzo ili kuishawishi Dortmund ikubali kupunguza bei hiyo na kukubali kupokea walau Pauni 40 milioni jambo ambalo linaonekana kuwa gumu.

Chelsea imevutiwa sana na staa huyu kutokana na kiwango chake akiwa katika timu ya Dortmund ambapo kwa msimu uliopita alicheza mechi 49 za michuano yote, akafunga mabao 12  na kutoa asisti tano.

Mkataba wa sasa wa  Gittens unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Alejandro Garnacho

MANCHESTER United inaweza kukubali ofa ya takribani Pauni 45 milioni kutoka kwa timu inayohitaji saini ya winga wao wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 20, Alejandro Garnacho katika dirisha hili.

Garnacho ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu uliopita alicheza mechi 58 za michuano yote na kufunga mabao 11.


Johan Bakayoko

NEWCASTLE imewaweka katika rada zao wachezaji kibao akiwamo winga wa PSV Eindhoven na timu ya taifa ya Ubelgiji, Johan Bakayoko, mwenye umri wa miaka 22, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Karim Adeyemi, kama mpango mbadala ikiwa itashindwa kuipata huduma ya winga wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya Sweden, Anthony Elanga, mwenye umri wa miaka 23.


Tyrell Malacia

HADI sasa Manchester United haijapokea ofa yoyote kutoka kwa timu zinazohitaji huduma ya beki wake wa kushoto wa kimataifa wa Uholanzi, Tyrell Malacia, mwenye umri wa miaka 25, ambaye alisaidia PSV Eindhoven kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uholanzi akiwa kwa mkopo msimu uliopita.

Mkataba wa Malacia unatarajiwa kumalizika mwakani.


Thierno Barry

EVERTON ipo katika mazungumzo na Villarreal kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22, Thierno Barry, ambaye wanahitaji huduma yake katika dirisha hili.

Barry ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, katika mkataba wake ana kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 34 milioni.


Alvaro Carreras

MABOSI wa Benfica wamefichua kuwa hadi sasa bado hawajapokea ofa kutoka kwa Real Madrid licha ya timu hiyo kuhusishwa na beki wa kushoto wa Hispania, Alvaro Carreras, mwenye umri wa miaka 22, ambaye alijiunga na wababe hao wa Jiji la Lisbon mwaka jana akitokea Manchester United. Mkataba wa sasa wa Carreras unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Francisco Conceicao

UVENTUS imeweka kipaumbe cha kwanza cha kumsajili staa wa FC Porto, Francisco Conceicao katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kabla ya kumgeukia winga wa Manchester United, Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 25. Awali, ilielezwa Juventus kipaumbele chao ilikuwa ni Sancho lakini inaonekana kiasi cha pesa kinachohitajika na Man United ni kikubwa zaidi.


Andreas Christensen

AC Milan imeanza mazungumzo na wawakilishi wa Barcelona kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa timu hiyo na Denmark, Andreas Christensen, 29, katika dirisha hili. Christensen, amepewa ruhusa ya kuondoka katika dirisha hili ikiwa atapata timu itakayokuwa tayari kumsajili. Barca tayari ina mabeki wakati watano katika kikosi chao.