Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca bado yamtaka Kane akamrithi Lewandowski

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Barca imevutiwa zaidi na Kane kwani mbali ya uwezo wake, mkataba wake unaweza kuvunjwa kwa Pauni 57 milioni ifikapo mwisho wa msimu huu, kiasi ambacho Barca hawaoni kama ni kikubwa.

BARCELONA inamwangalia straika wa Bayern Munich na timu ya taifa ya England, Harry Kane, 32, kama mbadala wa mshambuliaji wao wa kimataifa wa  Poland, Robert Lewandowski, 37, ambaye ataondoka mwisho wa msimu huu.

Barca imevutiwa zaidi na Kane kwani mbali ya uwezo wake, mkataba wake unaweza kuvunjwa kwa Pauni 57 milioni ifikapo mwisho wa msimu huu, kiasi ambacho Barca hawaoni kama ni kikubwa.

Hata hivyo, Kane mwenyewe ameweka wazi hana mpango wa kuondoka kwa sasa lakini watu wake wa karibu wanadai anavutiwa sana na Barcelona.

Mkataba wake wa sasa na Bayern unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote, akafunga mabao 23 na kutoa asisti tatu.

Hata hivyo, changamoto kubwa kwa Barca kushindwa kukamilisha dili hilo, inaweza kuwa mshahara wa Kane wa Euro 480,000 anaoupata kwa sasa.

Ili kumuingiza Kane katika mfumo ikiwa itamsajili kwanza itatakiwa kumlipa mshahara wa chini ya hapo au ikishindikana, ikimlipa mshahara sawa na huo itatakiwa kuondoa wachezaji wasiopungua wawili ili kuendana na sheria za La Liga za masuala ya fedha.


Adam Wharton

CHELSEA imepanga kupiga hodi kwa majirani zao Crystal Palace katika dirisha lijalo la majira ya baridi ili kuipata huduma ya kiungo wa klabu hiyo na timu ya taifa ya England,   Adam Wharton, 21. Wharton ambaye pia amejumuishwa katika kikosi cha England kilichoingia kambini ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Palace tangu msimu uliopita na mbali ya Chelsea, Manchester United pia imeoyesha nia ya kuhitaji huduma yake. Kuna uwezekano mkubwa nyota huyo akaondoa Palace dirisha lijalo.


Mike Maignan

JUVENTUS ina matumaini makubwa ya kumsajili kipa wa AC Milan, Mike Maignan katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika. Maignan mwenye umri wa miaka 30, pia anahusishwa na Chelsea ambayo inatafuta kipa kwa sababu hairidhishwi na kiwango cha Roberto Sanchez ambaye ndio kipa wao namba moja kwa sasa na msimu huu imekuwa ikiruhusu mabao na hivyo kuwa na panda shuka katika msimamo wa Ligi Kuu England.


Rodrygo

HADI sasa Chelsea bado haijatuma ofa yoyote Real Madrid ya kumsajili mshambuliaji wao, Rodrygo, 24. Staa huyu ambaye anataka kuondoka Madrid kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza,  yupo pia katika rada za timu mbalimbali za England ikiwemo Manchester City na Tottenham. Hata hivyo, changamoto kubwa inayosabªbisha vigogo hao kurudi nyuma ni ada ya uhamisho ambayo Madrid inaihitaji kuwa kubwa.


Kenan Yildiz

JUVENTUS imefeli kufikia makubalino ya kumsainisha mkataba mpya mshambuliaji wao wa kimataifa wa Uturuki, Kenan Yildiz, 20. Staa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2029,  anawindwa na Arsenal, Chelsea na Real Madrid. Juventus imekuwa ikipambana kutaka kumpa mkataba mpya ili kufuta kabisa matumaini ya timu zinazomhitaji lakini mpango huo unadaiwa kufeli kutokana na hitaji la mshahara la fundi huyo.


Endrick

REAL al Madrid inamalizia kufanya makubaliano na Olympique Lyon ambayo imeomba kumsajili straika wa kimataifa wa Brazil, Endrick mwenye umri wa miaka 19 dirisha lijalo. Timu nyingi zimeonyesha nia ya kumtaka kinda huyu lakini Madrid imeamua kumpeleka Lyon baada ya klabu hiyo kuwasilisha mpango mzuri unaoonyesha atapata nafasi kubwa ya kucheza kikosi cha kwanza na kuendeleza kiwango chake.


Kobbie Mainoo

MANCHESTER United imepanga kwanza kusajili kiungo mwingine dirisha lijalo la majira ya baridi kabla ya kumwachia Kobbie Mainoo, 20, kwa mkopo. Staa huyu ambaye anawindwa sana na Napoli na Leeds United amekuwa akiomba kuondoka tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini mabosi wa Man United hawataki kumruhusu.


Andreas Christensen

BEKI wa kimataifa wa Barcelona, Andreas Christensen, 29, anataka kuendelea kusalia klabuni hapo na kusaini mkataba mpya wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu ujao. Hata hivyo, staa huyu ameweka wazi bado hajafikia makubaliano yoyote ya kusaini mkataba mpya na vigogo wa Barca na bado hajajua ikiwa ataongezwa au ataachwa.