Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea bado inapambana kwa Alejandro Garnacho

TETESI Pict
TETESI Pict

Muktasari:

  • Garnacho ni mmoja kati ya wachezaji ambao Man United ipo tayari kuwauza katika dirisha hili lakini inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni kama ada yake ya uhamisho.

CHELSEA bado inashinikiza kutaka kuipata saini ya winga wa Manchester United na timu ya taifa Argentina, Alejandro Garnacho katika dirisha hili.

Garnacho ni mmoja kati ya wachezaji ambao Man United ipo tayari kuwauza katika dirisha hili lakini inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni kama ada yake ya uhamisho.

Chelsea haitaki kulipa pesa zote hizo na sasa inajaribu kufanya mazungumzo ili kupunguziwa bei na iweze kufanikisha usajili huo.

Garnacho mwenye umri wa miaka 21, anadaiwa kuwa na uhitaji sana wa kutua  Stamford Bridge baada ya kuhakikishiwa nafasi ya kucheza na Enzo Maresca.

Fundi huyu wa kimataifa wa Argentina amekuwa katika orodha ya wachezaji ambao Chelsea ilihitaji kuwasajili tangu dirisha la majira ya baridi.

Mbali ya Chelsea, taarifa kutoka talkSPORT zinafichua kuwa Chelsea inajiandaa pia kuwasilisha ombi kwenda RB Leipzig, kwa ajili ya kuipata huduma ya kiungo Xavi Simons, ambaye anaweza kucheza kama namba 10 au kama winga.

Kocha wa Chelsea, Maresca anahitaji sana huduma ya Garnacho kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chake kwani anaamini anaendana na mifumo yake.

Mkataba wa sasa wa winga huyo ambaye hatakiwi United, unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Amine Adli

WOLVES imefikia hatua nzuri katika mazungumzo ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa  Bayer Leverkusen na Morocco, Amine Adli, mwenye miaka 25, lakini kinachoonekana kuwa kikwazo ni kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kinachotakiwa na klabu yake.

Tovuti ya Bild imefichua kwamba, Leverkusen inahitaji takribani Euro 30 milioni ili kumuuza Adli ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Alvaro Morata

ALVARO Morata yupo kwenye matatizo makubwa Galatasaray baada ya kushindwa kuripoti mazoezini kwa siku mbili mfululizo, huku kukiwa na mkwamo wa uhamisho anaolazimisha wa kutaka kwenda katika klabu mpya ya Como iliyopanda daraja kwenda Serie A, ambayo inaripotiwa kuwa tayari imefikia makubaliano na mchezaji huyo. Hata hivyo, Galatasaray, ambako Morata yupo kwa mkopo hadi Januari 2026, imekataa kuidhinisha kuondoka kwake.


Sam Johnstone

BURNLEY imefikia makubaliano ya kumsajili kipa wa Wolves ambaye ni raia wa England, Sam Johnstone, mwenye unri wa miaka 32 akawe mbadala wa James Trafford, aliyejiunga na Manchester City katika dirisha hili.

Johnstone mwenyewe anadaiwa kuwa ameshafikia makubaliano binafsi na mabosi wa Burnely na amevutiwa sana na mpango uliowekwa mezani na Burnley.

Mkataba wa Trafford unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu uliopita alicheza mechi 10 za michuano yote.


Michael Cooper

WEST Ham inatarajiwa kuwasilisha ofa kwenda Sheffield United, hivi karibuni ili kuipata huduma ya kipa wa timu hiyo, Michael Cooper, mwenye umri wa miaka 25 katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Akiwa na Sheffield katika mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza England msimu uliopita, Cooper alicheza mechi 46 za michuano yote na kuruhusu mabao 35 huku kati ya hizo, mechi 23 hakuruhusu bao hata moja.


Max Alleyne

BEKI wa kati wa Manchester City ambaye ni raia wa England, Max Alleyne anaweza kuondoka kwa mkopo wa msimu mzima katika dirisha hili la majira ya kiangazi kwenda Watford ambayo imeanza mazungumzo ya kutaka kumsajili hivi karibuni. Staa huyu mwenye umri wa miaka 20, ni miongoni mwa wachezaji ambao hawana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Man City.


Leo Castledine

KIUNGO wa Chelsea na timu ya taifa ya England chini ya miaka 19, Leo Castledine anatarajiwa kujiunga na Huddersfield Town kwa mkopo wa msimu mmoja katika dirisha hili. Castledine ambaye msimu uliopita alicheza mechi 27 za michuano yote na kufunga mabao mawili, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Rob Holding

BEKI wa Crystal Palace, Rob Holding, 29, anatarajiwa kuondoka klabuni hapo katika dirisha hili la majira ya kiangazi kwenda Colorado Rapids inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani.

Kabla ya kufikia makubaliano ya kumsajili staa huyu Colorado ilikuwa katika vita kali dhidi ya Sheffield United na Wrexham zinazoshiriki Ligi Kuu Marekani.