Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cesc Fàbregas kocha bora SERIE A 2025/26 

FABREGAS Pict

Muktasari:

  • Fàbregas amepata heshima hiyo kubwa baada ya kuiongoza klabu hiyo kupata matokeo yaliyoshangaza wengi na kuleta ushindani mkubwa, jambo lililothibitisha uwezo wake wa mbinu na uongozi nje ya uwanja kama kocha chipukizi barani Ulaya.

Kiungo wa zamani wa Arsenal na Barcelona, Cesc Fàbregas, ametunukiwa tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kufuatia msimu wake wa kihistoria na wa kipekee akiwa na klabu ya Como. 


Fàbregas amepata heshima hiyo kubwa baada ya kuiongoza klabu hiyo kupata matokeo yaliyoshangaza wengi na kuleta ushindani mkubwa, jambo lililothibitisha uwezo wake wa mbinu na uongozi nje ya uwanja kama kocha chipukizi barani Ulaya.

Mafanikio hayo yanazidi kumweka Fàbregas kwenye ramani ya makocha wenye mustakabali mzuri wa baadae katika ulimwengu wa soka, huku mashabiki na wachambuzi wengi wakisifu mtindo wake wa uchezaji wa kuvutia na jinsi alivyobadili morali ya kikosi cha Como. 

Tuzo hii inakuja kama uthibitisho wa kazi kubwa aliyoifanya klabuni hapo na inatarajiwa kuwa chachu ya mafanikio makubwa zaidi kwa klabu hiyo katika msimu unaofuata wa ligi.

Cesc Fàbregas ametangazwa kuwa Kocha Bora wa Mwaka wa Serie A baada ya kuwapiku makocha wazoefu nchini Italia, akiwemo Simone Inzaghi (Inter Milan), Gian Piero Gasperini (Atalanta), na Thiago Motta (Juventus). 

Katika msimu uliopita, Fàbregas aliiongoza Como 1907 kupata ushindi katika mechi 22 kwenye mashindano yote. Kikosi chake kilionyesha soka la kuvutia, kushambulia kwa kasi, na nidhamu ya hali ya juu uwanjani, jambo lililomfanya aaminike haraka na mashabiki pamoja na uongozi wa timu hiyo.

Mafanikio makubwa zaidi yaliyompa tuzo hiyo ni pamoja na kuifikisha Como katika nafasi ya nne (4) kwenye msimamo wa Serie A. Hatua hiyo iliyoiwezesha klabu hiyo kupata tiketi ya kihistoria ya kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League).