Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick: Naziba masikio

CARRICK Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo ya Carrick imekuja baada ya Manchester United kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Leeds United kwenye Uwanja wa Elland Road, matokeo aliyoyatafsiri kuwa mwanzo mpya kwa kikosi chake licha ya kukiri kuwa mwenendo wa timu hiyo hauwaridhishi.

LEEDS, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema amelazimika kujikinga na kelele za nje zinazozunguka klabu hiyo katika kipindi kigumu, akitumia mfano wa kuvaa 'headphones' ili kuepuka usumbufu na kuendelea kuielekeza timu yake katika majukumu ya uwanjani.

Kauli hiyo ya Carrick imekuja baada ya Manchester United kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Leeds United kwenye Uwanja wa Elland Road, matokeo aliyoyatafsiri kuwa mwanzo mpya kwa kikosi chake licha ya kukiri kuwa mwenendo wa timu hiyo hauwaridhishi.

United wamekuwa na wakati mgumu, wakifanikiwa kushinda mechi mbili pekee kati ya 10 zilizopita, rekodi ambayo Carrick amekiri kuwa haipendezi hata kidogo.

“Ndani ya klabu kumekuwa na utulivu, lakini wiki hii nimekuwa na headphones sikioni ili kuzima kelele za nje,” amesema Carrick.

Alieleza kuwa kabla ya mchezo huo aliwakumbusha wachezaji wake umuhimu wa pambano hilo, historia ya wapinzani wao na namna mashabiki wa Leeds wanavyolichukulia, akisisitiza kuwa kucheza ugenini katika mazingira hayo kunahitaji maandalizi na moyo wa kupambana.

CARR 01

Carrick amesema amefurahishwa na namna wachezaji wake walivyoikabili mechi hiyo, ingawa hakutaka kujisifu kupita kiasi kwa sababu hawakuondoka na pointi zote tatu.

“Hatupaswi kujisahau kwa sababu hatujashinda mchezo. Lakini, kwa kweli, nimehisi kama huu ni mwanzo mpya kwa namna tulivyo, kukubali hali yetu na kuchukua hatua za kuibadilisha,” ameongeza.


KELELE ZA NJE

Kabla ya mchezo huo, gumzo kubwa lilihusu beki wa Manchester United, Lisandro Martinez, ambaye aliripotiwa kutoa malalamiko makali dhidi ya viongozi wa klabu hiyo baada ya mchezo wa katikati ya wiki mjini Madrid.

Hata hivyo, Martinez alidumu uwanjani kwa dakika 45 pekee dhidi ya Leeds kabla ya kutolewa kutokana na jeraha la paja.

Licha ya sare hiyo, Manchester United bado inakabiliwa na changamoto ya kurejesha makali yake, huku Carrick akikiri kuwa hali ya timu hiyo haiwezi kufichwa kwa matokeo ya mchezo mmoja.

CARR 02

“Ninaelewa kuwa hali haiko vizuri ukiitazama kwa namna fulani, lakini sina shaka kwamba tunaweza kuanza kupata matokeo mazuri mfululizo,” amesema.

Ameongeza kuwa anafahamu ukubwa wa changamoto iliyopo na kwamba timu inahitaji kuwa imara, yenye umoja na inayoweza kuendelea kufanya mambo sahihi hata inapopitia kipindi kigumu.

Katika mchezo huo, Bryan Mbeumo aliipa Manchester United bao la kuongoza kipindi cha kwanza, kabla ya Dominic Calvert-Lewin kuisawazishia Leeds United muda mfupi baada ya mapumziko kwa kutumia mpira wa kona.

Bao hilo lilikuwa la tano kwa Calvert-Lewin msimu huu na kuendeleza mwanzo mzuri wa Leeds katika kampeni yao ya ligi.

Beki wa United, Harry Maguire, amesema timu yake ilifanya makosa kwa kuruhusu bao la kusawazisha kupitia mpira wa kutenga baada ya mapumziko, akisisitiza kuwa makosa ya aina hiyo yanaweza kugharimu matokeo muhimu.

CARR 03

“Ni jambo la kukatisha tamaa kufungwa bao kupitia mpira wa kutenga baada ya mapumziko. Unapokwenda kucheza kwenye viwanja kama hivi, hupaswi kuruhusu mabao ya namna hiyo,” amesema Maguire.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa hakuona tatizo katika umoja na ari ya kupambana ya wachezaji wa United, akieleza kuwa timu hiyo ilionekana kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kupata bao la ushindi katika dakika za mwisho.

Kwa upande wake, Calvert-Lewin amesema alilenga kuwasumbua mabeki wa United katika eneo la hatari na kutumia nafasi iliyojitokeza baada ya kusoma vizuri mwelekeo wa mpira.