Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maswali muhimu baada ya kauli ya Martinez Man Utd

MARTINEZ Pict

Muktasari:

  • Kutokana na hilo, haya ndiyo maswali muhimu yaliyoibuka na nini mustakabali wa Manchester United katika mashindano mbalimbali msimu huu licha ya kwamba nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alishaomba radhi?

MANCHESTER, ENGLAND: Baada ya Manchester United kufungwa mabao 2-0 na Atletico Madrid, beki wa kati Lisandro Martinez alimshambulia mkurugenzi wa masuala ya soka wa timu hiyo, Jason Wilcox, pamoja na viongozi wengine wa juu wa klabu hiyo katikati ya wiki hii na kuibua maswali kibao kuhusiana na maisha ndani ya kikosi hicho.

Martinez alisema: “Kwa sasa hatuna kikosi bora zaidi tukijilinganisha na timu nyingine kubwa. Natarajia uwekezaji zaidi, kwa asilimia 100. Natarajia mengi zaidi kutoka kwa mkurugenzi wetu wa ufundi, Jason Wilcox... Kufungwa na Atletico ni jambo baya sana. Inanibidi nijidhibiti sana, lakini hali hii inaakisi jinsi klabu yetu ilivyo kwa sasa.”

Kutokana na hilo, haya ndiyo maswali muhimu yaliyoibuka na nini mustakabali wa Manchester United katika mashindano mbalimbali msimu huu licha ya kwamba nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alishaomba radhi?


MART 01

MAONI YAKE YANAENDANA NA HISIA ZA WENZAKE?

Jibu fupi ni ndiyo. Gazeti la The Guardian la Uingereza linaelezwa kuwa uamuzi wa klabu kulenga kuwasajili viungo watatu Andrey Santos, Youri Tielemans na Carlos Baleba ulizua mshangao miongoni mwa wachezaji wa kikosi hicho kutokana na maeneo mengine ya timu kutofanyiwa maboresho katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi.

Carrick aliiongoza United kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita, licha ya kubakiwa na mechi 17 pekee za ligi wakati alipopewa jukumu hilo mwezi Januari, baada ya timu hiyo kutolewa katika mashindano mengine. Haja ya kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ni kubwa zaidi kwa sababu safu ya nyuma inayoundwa na Diogo Dalot, Martínez, Harry Maguire na Luke Shaw imekuwa pamoja tangu 2022.

Mkataba wa Martinez unamalizika mwakani, na inadaiwa kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 28 huenda asipewe mkataba mpya au klabu isitumie kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi. Kwa hiyo, wachezaji wenzake wanafahamu kuwa mlipuko wake wa hasira huenda pia umetokana na matarajio yake ya kuondoka klabuni hapo.


MART 02

WILCOX ANAPASWA KULAUMIWA KIASI GANI?

Akiwa mkurugenzi wa masuala ya soka wa United, Wilcox mwenye umri wa miaka 55 ana mamlaka makubwa, karibu ya mwisho, katika mambo yanayohusu soka, huku Sir Jim Ratcliffe, anayesimamia sera za michezo za klabu hiyo akiwa ndiye kiongozi pekee aliye juu yake katika eneo hilo. Ikiwa lawama za uamuzi wa klabu zinaishia kwa viongozi wakuu, basi dirisha la hivi karibuni la usajili lilikuwa jukumu la Wilcox.

Hili ni tukio la hivi karibuni katika orodha ya makosa yanayohusishwa na kipindi chake akiwa United.

Mojawapo linahusu kipindi ambacho Dan Ashworth, mtangulizi wa Wilcox, alikuwa katika likizo maalumu ya kutoruhusiwa kufanya kazi  baada ya kuondoka Newcastle, katika nusu ya kwanza 2024. Wakati huo, Wilcox aliwahoji watu waliokuwa wakifuatiliwa kuchukua nafasi ya kocha Erik ten Hag kabla ya kufanya uamuzi wa kushangaza kwamba kocha huyo mkuu alipaswa kuendelea kubaki. Ten Hag alisaini mkataba mpya, lakini alifutwa kazi katika msimu huohuo.

Tukio jingine linahusu mgogoro kati ya Wilcox na kocha Ruben Amorim, ambaye alikuwa amemteua kuchukua nafasi ya Ten Hag. Baada ya kutofautiana, Amorim alidai mkurugenzi huyo  alimwambia alipaswa kubadili mfumo wake alioupenda wa 3-4-3.

“Nilikuja hapa kuwa meneja wa Manchester United, siyo kuwa kocha wa Manchester United,” alisema Amorim baada ya sare ya mabao 1-1 dhidi ya Leeds Januari 4. Wakati huo, cheo chake rasmi kilikuwa kocha mkuu. Alifutwa kazi siku iliyofuata.

Wilcox aliwahi kufanya kazi na Omar Berrada, ambaye sasa ni mtendaji mkuu wa Man United. Berrada alipanda vyeo hadi kuwa mkuu wa shughuli za soka, huku Wilcox akiteuliwa kuwa mkurugenzi wa akademi. Wilcox alihamia Southampton na kuwa mkurugenzi wa masuala ya soka kuanzia 2023 hadi Aprili 2024, alipohamia United baada ya kuvutwa na Berrada. Kutokana na historia hiyo, uzoefu wake katika kusimamia masuala ya soka katika kiwango cha juu sasa unafuatiliwa kwa karibu.


MART 03

CARRICK ANAWAJIBIKA KWA KIASI GANI?

Uwezo wa kocha Carrick, 45, kufanikiwa unategemea kwa kiasi kikubwa ubora wa kazi ya Wilcox, hasa katika usajili. Kwa hiyo hawezi kubebeshwa lawama zote kutokana na hali mbaya ya timu ambayo imekusanya pointi sita pekee katika mechi sita za ligi ikishinda mara mbili katika mashindano yote msimu huu.

Hata hivyo, kwa maana ya majukumu yake kama kocha mkuu, Carrick anatakiwa kutumia vizuri rasilimali alizonazo na kuhakikisha timu inapiga hatua kupitia mazoezi. Katika siku za mechi, hakuna sababu ya kutosha inayoweza kuhalalisha jinsi United inavyocheza bila mshikamano, takwimu duni za umbali wa kukimbia uwanjani na kushindwa kutumia faida ya kuwa na wachezaji wengi zaidi mara mbili.

Hali hiyo ilionekana katika kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Man City na sare ya 1-1 dhidi ya Tottenham Jumamosi iliyopita, ambapo wapinzani wao walikuwa na wachezaji 10 uwanjani.

Wachezaji wanamchukuliaje Carrick? Kwa mujibu wa Santos, wachezaji wanamuunga mkono.

“Tuna imani na meneja, tuna imani na benchi lote la ufundi, na tuna imani na sisi wenyewe kama wachezaji. Tuko katika kipindi kigumu, lakini tunapaswa kufanya kazi ili kubadili matokeo haya,” alisema baada ya mechi dhidi ya Atletico.


MART 04

UMOJA NA NIDHAMU UNITED VINAPOTEA?

Ushahidi wa yaliyotajwa hapo juu mwingine unaonyeshwa kupitia ujumbe wa winga Amad Diallo aliouchapisha kwenye mtandao wa Snapchat baada ya kipigo dhidi ya Atletico, alipodai: “Ni aibu kubwa sana; sina maneno (ya kusema).”

Kwa hiyo, United sasa ina mchezaji aliyewahi kutwaa Kombe la Dunia, Martinez akimlenga Wilcox kwa shutuma ambazo pia zinawahusisha kwa maana pana Ratcliffe na Berrada. Wakati huohuo, mchezaji mwingine mwenye uzoefu mkubwa, Diallo, ametumia lugha ya kulaani kwa namna ambayo haieleweki wazi anachokilenga.

Hali hiyo imeongeza hisia kwamba klabu inakabiliwa na mgogoro mkubwa, kwa sababu haijulikani kama neno “aibu” alilotumia Diallo lilimaanisha kiwango cha uchezaji wa timu, mashambulizi ya maneno ya Martinez, kikosi ambacho mwenzake alidai hakina ubora wa kutosha au jambo jingine tofauti.

Hali hiyo inaonekana pia uwanjani. United imekimbia jumla ya kilomita 671.4 katika mechi za Ligi Kuu England, ikiwa ni rekodi ya tano kutoka mwisho kwa timu zinazokimbia umbali mdogo zaidi. Arsenal ndiyo inayoongoza kwa umbali mkubwa zaidi, ikiwa na kilomita 716.2.

Katika idadi ya mbio za kasi, United imefanya mbio 581 pekee, ikiwa ya nne kutoka mwisho. Brentford ndiyo inayoongoza kwa kufanya mbio hizo mara nyingi zaidi, ikiwa na jumla ya 765.