Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu ya Wanawake kuanza Oktoba 28

WPL Pict

Muktasari:

  • Kutoka kuwa sintofahamu ya ratiba iliyokuwa ikiwapa presha makocha na viongozi wa klabu kuhusu maandalizi ya msimu mpya, hatimaye Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka wazi ratiba kamili na kuondoa kizungumkuti kilichokuwa kimetanda.

SAFARI ya kutafuta malkia mpya wa soka la wanawake nchini inaanza rasmi Oktoba 28, 2026, wakati Ligi Kuu ya Wanawake Bara (WPL) msimu wa 2026/27 ikitarajiwa kufungua pazia la vita ya kuwania ubingwa kwa mechi sita kupigwa katika viwanja mbalimbali.

Kutoka kuwa sintofahamu ya ratiba iliyokuwa ikiwapa presha makocha na viongozi wa klabu kuhusu maandalizi ya msimu mpya, hatimaye Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka wazi ratiba kamili na kuondoa kizungumkuti kilichokuwa kimetanda.

Msimu huu unatarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake huku timu 12 zikianza safari ya kusaka pointi zitakazozipa nafasi ya kutwaa taji hilo, katika ligi ambayo kila msimu imekuwa ikiibua vipaji vipya.

Mechi zote za ufunguzi wa msimu zitapigwa kuanzia saa 10:00 jioni katika viwanja tofauti. Mabingwa watetezi Simba Queens, wataanzia kampeni yao ugenini dhidi ya Kilimanjaro Wonders ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki ligi ikipanda kutoka Ligi ya Mkoa, katika Uwanja wa Ushirika, Moshi.

WP 01

Simba Queens inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na morali baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga JKT Queens bao 1-0 katika fainali iliyochezwa Oktoba 3, 2026. Hata hivyo, mchezo huo hautakuwa mwepesi kwani Kilimanjaro Wonders itakuwa inasaka kuweka historia na kuonyesha .

Kibarua kingine kitakuwa Mkoani Mara, ambapo Yanga Princess watacheza dhidi ya Bunda Girls mechi itapigwa Uwanja wa Karume.

JKT Queens, wataanza safari yao ya kusaka heshima na kurekebisha makosa ya msimu uliopita itakapokipiga na Geita Queens katika Uwanja wa Nyamkumbu.


WP 02

MECHI ZINGINE

Fountain Gate Princess vs Mashujaa Queens (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma)

Kilimanjaro Wonders vs Simba Queens (Uwanja wa Ushirika, Moshi)

Bunda Girls vs Yanga Princess (Uwanja wa Karume, Mara)

Geita Queens vs JKT Queens (Uwanja wa Nyamkumbu, Geita)

Ceasiaa Queens vs Alliance Girls (Uwanja wa Samora, Iringa)

Tausi FC vs Bunda Queens (Uwanja wa Nyamagana, Mwanza)