Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick, Fernandes wakutana kutuliza upepo mbaya Man United

WAKUTANA Pict

Muktasari:

  • Fernandes, mwenye umri wa miaka 32, hakutumika katika mchezo ambao United ilifungwa mabao 3-0 na Bournemouth Jumapili iliyopita. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno aliachwa benchi baada ya kukosoa mbinu za Carrick kufuatia kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Como katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LONDON, ENGLAND: Kocha wa Manchester United, Michael Carrick, na nahodha wake, Bruno Fernandes wamezungumza kwa faraghani kwa lengo la kumaliza tofauti zao kabla ya kikosi hicho kusafiri kwenda kukabiliana na Chelsea katika Ligi Kuu England.

Fernandes, mwenye umri wa miaka 32, hakutumika katika mchezo ambao United ilifungwa mabao 3-0 na Bournemouth Jumapili iliyopita. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno aliachwa benchi baada ya kukosoa mbinu za Carrick kufuatia kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Como katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyozungumza na BBC Sport, wawili hao walikutana faraghani katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo Jumanne, wakilenga kuweka wazi malalamiko na kutafuta suluhu ya tofauti zao.

Hata hivyo, haijafahamika kama Fernandes, aliyeteuliwa kuwa nahodha wa United mwaka 2023, aliomba radhi kwa kauli zake za kuikosoa mbinu za kocha huyo.

WAKU 01

United inajiandaa kuvaana na Chelsea Jumamosi kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, mchezo unaotarajiwa kuanza saa 12:30 jioni kwa saa za Tanzania. Fernandes anaweza kurejea katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo.

Carrick alitarajiwa kufutwa kazi baada ya kichapo dhidi ya Bournemouth, lakini uongozi wa klabu hiyo umeamua kumpa nafasi ya kujaribu kubadili hali ya timu, licha ya United kushika nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 alipata habari nyingine njema Jumatano baada ya kiungo Kobbie Mainoo kurejea mazoezini kufuatia kukaa nje kwa wiki mbili kutokana na jeraha.

United imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya mechi nane za Ligi Kuu England msimu huu. Hata hivyo, uongozi wa klabu hauamini kuwa Carrick ndiye anayepaswa kubeba lawama zote kwa mwenendo huo.

WAKU 02

Viongozi waandamizi wa United wanaamini kuwa kikosi hicho kina uwezo wa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini wachezaji wamekuwa wakifanya chini ya kiwango chao na wanapaswa kuwajibika kwa sehemu ya hali hiyo.

Mchezaji mmoja wa United aliiambia BBC Sport: “Hisia zilizopo ni kwamba sote tunataka kurekebisha hali hii. Wachezaji, benchi la ufundi na kila mmoja.”

Pamoja na uamuzi wa kuendelea na Carrick kwa sasa, vyanzo vya BBC Sport vimedai kuwa United tayari imeorodhesha majina ya aliyekuwa kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na Bayern Munich, Julian Nagelsmann, kama wanaoweza kuchukua nafasi ya Carrick.

WAKU 03

Iwapo United itaamua kumteua Howe, italazimika kulipa fidia ya mamilioni ya pauni kwa Newcastle, klabu yake ya zamani. Kwa upande wa Nagelsmann, kwa sasa hana klabu.