Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick awatetea nyota Man United

CARRICK Pict

Muktasari:

  • Mbali na Neville, mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Wayne Rooney, naye ameongeza makali ya ukosoaji kwa kusema wachezaji hao wanatakiwa kufanyishwa mazoezi maalumu ili kubadili kiwango chao.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick amepinga vikali madai baadhi ya wachezaji wake hawana nidhamu ya kitaaluma, akisisitiza bado ana imani nao licha ya timu hiyo kukumbwa na wimbi kubwa la ukosoaji kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka.

Carrick ametoa kauli hiyo baada ya shutuma zilizotolewa na aliyekuwa nyota wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, ambaye alidai baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho hawazingatii muda sahihi wa kulala wala kula chakula kinachofaa kwa mwanamichezo.

Mbali na Neville, mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Wayne Rooney, naye ameongeza makali ya ukosoaji kwa kusema wachezaji hao wanatakiwa kufanyishwa mazoezi maalumu ili kubadili kiwango chao.

Kauli hizo zimekuja wakati Carrick akiwa kwenye presha kubwa ya kuokoa kibarua chake baada ya Manchester United kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Bournemouth kwenye Uwanja wa Old Trafford Jumapili iliyopita.

CARR 01

Kichapo hicho kiliwaumiza mashabiki wa United, ambao walimshangilia Carrick alipokuwa akielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, kabla ya kugeuza hasira zao kwa wachezaji.

Akijibu swali kuhusu madai ya kutokuwepo kwa weledi wa kitaaluma kwa baadhi ya wachezaji wake, Carrick amesema hajakutana na tabia hizo ndani ya kikosi chake.

“Hapana, sijakutana na hali hiyo. Gaz (Gary Neville) huwa anasema mambo mengi!” amesema Carrick.

Baada ya uongozi wa United kuamua kumpa Carrick muda zaidi wa kubadilisha mwenendo wa timu hiyo, kocha huyo alikutana na wachezaji katika uwanja wa mazoezi wa Carrington Jumanne, ambapo walijadili hali ya timu na hasira za mashabiki.

CARR 02

Carrick amesema lengo la mazungumzo hayo lilikuwa kuwahakikishia wachezaji kuwa bado yupo pamoja nao na hatakubali kuwatenga katika kipindi hicho kigumu.

“Nilitaka waelewe kuwa mimi nipo pamoja nao. Hakuna namna ninavyoweza kujitenga nao,” amesema.

Ameongeza: “Ninaheshimu na kuthamini namna mashabiki walivyoonyesha hisia zao. Nipo pamoja nao na tutapitia hali hii kwa pamoja.

“Kwa upande wangu nilikuwa na hisia tofauti. Kuthaminiwa na mashabiki, kuona uhusiano na heshima waliyonayo kwangu ni jambo ninalolichukulia kwa uzito mkubwa.

CARR 03

“Lakini hilo halimaanishi kuwa nilijisikia vizuri kwa sababu bado nipo pamoja na wachezaji kwa asilimia 100.”

Carrick alisisitiza kuwa kikosi hicho kinapaswa kuwajibika kwa pamoja, akieleza kuwa yeye ndiye kocha wa wachezaji hao na Manchester United ndiyo klabu yake, hivyo hakuna sababu ya kujitenga na changamoto zinazowakabili.

“Hawa ni wachezaji wangu, hiki ni kikosi changu na hii ni klabu yangu. Tunapaswa kukabiliana na hali hii kwa pamoja.

“Hata mashabiki ni sehemu ya jambo hili. Najua mambo ni magumu kwa sasa na ninaelewa hisia zao. Tukifanikiwa kuvuka kipindi hiki, tutakuwa imara zaidi kama klabu nzima,” amesema.

CARR 04

Kocha huyo pia amekiri kuwa United inahitaji kuboresha kiwango chake uwanjani na kuonyesha dhamira kubwa zaidi ili kurejesha imani ya mashabiki.

Wakati huohuo, mashabiki wa United wameelekeza lawama zao kwa wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazer, Sir Jim Ratcliffe, pamoja na mtendaji mkuu Omar Berrada na mkurugenzi wa soka Jason Wilcox.

Akizungumzia mazungumzo yake na wachezaji, Carrick amesema si kila wakati mawasiliano ndani ya klabu yanakuwa ya furaha, kwani wakati mwingine ukweli mchungu lazima usemwe ili kupata suluhisho.

“Si kila mazungumzo huwa mazuri na yenye kufurahisha. Hilo linaweza kuwa kati yangu na wachezaji, mimi na Jason, Omar au hata wamiliki wa klabu. Wakati mwingine tunahitaji kuzungumza ukweli mchungu ili kujua namna ya kusonga mbele,” amesema.