Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manqoba ashtua! Ataka 10 Yanga

YANGA Pict


YANGA imefanikiwa kuanza vyema msimu wa 2026-2027 kwa kushinda ugenini ikiwapa furaha mashabiki wake, lakini kocha wa timu hiyo, Manqoba Mngqithi hajafurahi sana huku akitangaza sasa kuna kumi tu zimesalia ili mambo yawe moto zaidi.


Ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Namungo katika mechi ya Ligi Kuu Bara juzi Jumamosi, umeipa morali Yanga, ikianza kwa kishindo hesabu za kutetea ubingwa wa ligi hiyo kwa mabao ya beki Chadrack Boka, kiungo Maxi Nzengeli na mshambuliaji Peter Shalulile.


Akizungumza na Mwanaspoti, Manqoba amesema, licha ya kikosi chake kuanza na ushindi mzuri, lakini bado hakijacheza kwa kiwango ambacho anatamani kuona kikicheza ambapo hawakuwa na ubora ambao wanastahili kuwa nao.

YANG 01

Manqoba raia wa Afrika Kusini, amesema kutokana na kikosi chake kutopata muda wa kutosha wa maandalizi ya msimu, kinahitaji angalau mechi 10 ili kuendelea kupata ubora anaoutaka.

“Ni furaha kuona timu imeanza kwa ushindi, hii itawaimarisha kwenye hali ya kujiamini lakini ukiniuliza mimi naona bado haijaweza kucheza kwenye kiwango ambacho tunastahili kucheza, tuna safari kidogo ya kufanya maboresho,” aslisema Manqoba.

“Unafahamu kwamba hatukupata muda wa kutosha wa maandalizi ya mwanzo wa msimu, tulifanya kitu lakini sio kwa ukubwa, tunahitaji angalau mechi 10 hivi baada ya hapo nadhani tutakuwa tumeimarika kwa ubora kwa kiwango kikubwa.

YANG 02

Manqoba aliongeza kuwa, licha ya Yanga kupata mabao matatu dhidi ya Namungo, bado hawakuonyesha njaa ya kupata ushindi mkubwa kulingana na nafasi ambazo walizitengeneza kwenye mechi hiyo.

“Nikweli tumefanya vizuri kufunga mabao matatu lakini nikiwaheshimu wapinzani wetu ni kwamba tuliwazidi na kuwa juu yao kwa kiwango kikubwa, tulitengeneza nafasi nyingi sana lakini hatukuwa na njaa ya kutaka ushindi mkubwa zaidi.

“Tulistahili ushindi mkubwa zaidi ya huu, tungeweza kufunga kuanzia mabao sita au saba, bado tuna nafasi ya kuendelea kurekebisha haya kwenye eneo la mazoezi lakini pia kupitia mechi kama hizi, sio rahisi lakini tutafanikisha,” amesema kocha huyo ambaye ameanza msimu wa 2026-2027 kwa kuipa Yanga Ngao ya Jamii, Agosti 12, 2026 kwa kuifunga Simba bao 1-0.

YANG 03

Yanga baada ya kuanzia ugenini, sasa inarudi nyumbani kuikaribisha Coastal Union katika mechi itakayochezwa Alhamisi Agosti 20, 2026 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Manqoba anafahamu kwamba, ana jukumu la kuiongoza Yanga kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo timu hiyo imeuchukua mara tano mfululizo kuanzia 2021-2022 huku ikiwa ndiyo iliyobeba mara nyingi zaidi kihistoria ikifanya hivyo mara 32.