Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Camavinga anauzwa, weka ofa yako ubaoni

Muktasari:

  • Camavinga, 22, alijiunga na Real Madrid akitokea Rennes ya Ufaransa, Agosti 2021 na tangu wakati huo ameichezea Los Blancos mara 166 akifunga mabao matatu na kuasisti mara tisa.

REAL Madrid imeripotiwa kufungua milango ya kumpiga bei kiungo Eduardo Camavinga kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi endapo kama kutakuwa na ofa nzuri ubaoni.

Camavinga, 22, alijiunga na Real Madrid akitokea Rennes ya Ufaransa, Agosti 2021 na tangu wakati huo ameichezea Los Blancos mara 166 akifunga mabao matatu na kuasisti mara tisa.

Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akisumbuliwa sana na majeruhi msimu huu, ambapo alikosa mwanzo wa msimu kutokana na kuwa na tatizo la maumivu ya goti kabla ya kuwa nje kwa awamu mbili tofauti kwa matatizo ya maumivu ya misuli. Hilo limemfanya Camavinga amecheza mechi 10 tu kwenye La Liga msimu huu alitumika kutokea benchini katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City, Jumatano iliyopita. Dani Ceballos kwa sasa ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kucheza kwenye kiungo ya kati akimweka benchi Camavinga na sasa Real Madrid inasikilizia ofa ya kumuuza kabisa mwisho wa msimu.


Aleksandar Pavlovic

MANCHESTER United imeripotiwa kupanga kumtumia Marcus Rashford kama chambo ya kumnasa kiungo wa Bayern Munich, Aleksandar Pavlovic kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Rashford aliondoka Man United kwa mkopo kwenye dirisha la majira ya baridi kwenda kujiunga na Aston Villa hadi mwisho wa msimu na kocha wa miamba hiyo ya Villa Park, Unai Emery alisema kuna uwezekano wa kumchukua jumla staa huyo kwa ada ya Pauni 40 milioni. Lakini, Aston Villa inakabiliwa na tatizo la kifedha.


Rafael Leao

CHELSEA imeripotiwa imepata mzuka mkubwa kwenye mpango wao wa kufukuzia huduma ya fowadi wa AC Milan, Rafael Leao. Leao, 25, amekuwa kwenye mijadala ya kuhama kwa kipindi cha karibuni na sasa Chelsea inapewa nafasi kubwa ya kunyakua huduma ya winga huyo kwenye dirisha lijalo. Leao amekuwa na msimu mzuri kwenye Serie A akiwa na kikosi hicho cha Rossoneri, ambapo amefunga mabao matano na asisti tano katika mechi 22.


Mason Greenwood

BARCELONA imeripotiwa kuingia kwenye vita na klabu za Bayern Munich na Paris Saint-Germain kwenye mchakamchaka wa kunasa saini ya mshambuliaji wa Marseille, Mason Greenwood. Greenwood amevutia timu nyingi vigogo huko Ulaya kutokana na kile anachofanya kwenye klabu hiyo ya Ufaransa katika mikikimikiki ya Ligue 1. Winga huyo amecheza meci 22 katika kikosi cha Marseille msimu huu, akifunga mabao 14 na kuasisti mara tatu. Msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Getafe.


Cole Palmer

CHELSEA imeripotiwa kwamba huenda ikalazimika kumpiga bei staa wao Cole Palmer kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi kutokana na kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake. Kipengele hicho kinabainisha kwamba endapo kama Chelsea itashindwa kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, basi hawatakuwa na namna zaidi ya kumpiga bei Palmer endapo kama kuna timu iliyofuzu michuano hiyo itahitaji huduma yake.


Geovany Quenda

MANCHESTER United imeripotiwa kukubali kunasa saini ya kinda wa Sporting Lisbon, Geovany Quenda mwishoni mwa msimu huu ambapo klabu yake inataka ilipwe Pauni 50 milioni. Quenda, 17, ni kinda aliyeonyesha uwezo mkubwa wa kucheza upande wa kulia kwenye beki na winga na alipewa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Sporting na kocha wa sasa wa Man United, Ruben Amorim. Man United inasubiri Aprili ifike, ambapo atatimiza umri wa miaka 18 na hapo itapambana kunasa saini yake.


Jeremie Frimpong

LIVERPOOL inaripotiwa kupiga hesabu za kumnasa staa wa Bayer Leverkusen, Jeremie Frimpong ikimtazama kama mchezaji anayefaa kwenye kuvaa buti za beki wao wa kulia Trent Alexander-Arnold. Kinachoelezwa ni kwamba Alexander-Arnold yupo kwenye mipango ya kuachana na miamba hiyo ya Anfield, huku Real Madrid ikiripotiwa ndiko anakotaka kwenda mchezaji huyo, hivyo Liverpool inamtazama Frimpong kama mbadala wake, lakini saini yake kuipata itawaingiza kwenye vita kali na Manchester City.


Kyle Walker-Peters

LEEDS United imeripotiwa inamfuatilia kwa karibu beki wa Southampton, Kyle Walker-Peters ikitaka saini yake kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi. Beki huyo wa pembeni amekuwa kwenye kiwango bora kabisa kiasi cha kuzivutia timu nyingi zinazohitaji saini yake, ambapo timu za Leicester City na Everton nazo ziliwahi kuhusishwa na kuifukuzia huduma yake. Galatasaray pia iliwahi kuhitaji saini ya Walker-Peters.