Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno Fernandes ataka usajili mpya

Muktasari:

  • Nahodha huyo wa Man United alisema wachezaji wa timu hiyo walionyesha uvivu mkubwa katika mechi yao ya mwisho ya pre-season huko Marekani, ilipotoka sare ya 2-2 na Everton kwenye Uwanja wa Mercedes-Benz, licha ya kwamba imenyakua taji la Premier League Summer Series.

ATLANTA, MAREKANI: KIUNGO mbunifu wa Manchester United, Bruno Fernandes amesema timu hiyo inapaswa kufanya usajili wa mastaa wengine zaidi kabla ya msimu mpya kuanza.

Nahodha huyo wa Man United alisema wachezaji wa timu hiyo walionyesha uvivu mkubwa katika mechi yao ya mwisho ya pre-season huko Marekani, ilipotoka sare ya 2-2 na Everton kwenye Uwanja wa Mercedes-Benz, licha ya kwamba imenyakua taji la Premier League Summer Series.

Kabla ya sare hiyo, mechi mbili za kwanza, Man United ilishinda zote dhidi ya West Ham United na Bournemouth.

Fernandes, ambaye alicheza kwa dakika 90 katika mchezo huo wa Everton, alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti, lakini kikosi hicho cha kocha Ruben Amorim mara mbili kiliruhusu wapinzani kusawazisha na hivyo kutoka sare jambo lililomfanya nahodha Fernandes kutoa tamko.

“Tumebadilika, lakini bado hatujafika tunapotaka kuwa,” alisema Fernandes.

“Ni mchezo wa soka, siku zote unahitaji kucheza kwa moyo. Chochote kitakachokuwa kimetokea, basi kimetokea. Hakuna kitu cha ziada sana, ni kawaida tu kama ulivyo mchezo wenyewe.

“Tumekuwa na wakati mzuri kwenye ziara ya Marekani kwa sababu imetengeneza muunganiko mzuri na wachezaji. Lakini, kwenye mechi hii tulikuwa wavivu, tunahitaji kubadili hiyo hali. Sitaki kumsema yeyote, lakini klabu inapaswa kufanya kwa kadri inavyoweza juu ya masuala yanayozungumzwa. Sifahamu sana juu ya hilo, kwa sababu sijihusishi nayo. Lakini, kitu cha wazi kabisa, tunahitaji wachezaji wakuja kuleta ushindani.

“Tunahitaji viwango zaidi ili mapambano ya kupata namba kwenye kikosi cha kwanza yawe makubwa. Nadhani hicho ndicho klabu na kocha wanajaribu kukifanya na naamini tutapata mchezaji mmoja au wawili wapya wa kuja kusaidia hilo.”

Man United ilimaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita, nafasi ya chini zaidi iliyowahi kushika katika kipindi cha nusu karne na Fernandes anakiri kwamba hilo linapaswa kubadilika ili aibu isijirudie.

Kocha Amorim aliruhusu mazungumzo kama hayo ya Fernandes kuwapo kwenye kikosi chake ili kumfanya kila mchezaji kutambua kile ambacho Man United imelenga kufanya msimu huu katika kupambania mataji.

“Nafurahia kuona wachezaji nao wanaguswa kihisia,” alisema Amorim.

“Hilo linamaana wanaelewa hali halisi ilivyo. Ni kitu kizuri. Inafahamika kwamba kwenye timu hii kila kitu kuna kupanda na kushuka. Lakini, ninachotaka mimi ni upande wa kupanda kuliko huo mwingine."

Man United imekuwa ikihusishwa na mpango wa kumsajili straika Benjamin Sesko kutoka RB Leipzig, huku ikimsaka pia kipa wa Aston Villa, Emi Martinez, ambapo ikiwanasa hao Amorim atakuwa ametengeneza kikosi cha kibabe.

Kikosi cha ndoto Man United: E Martinez; Yoro, De Ligt, L Martinez; Dalot, Ederson, Fernandes, Dorgu; Mbeumo, Cunha, Sesko.