Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brighton ya tatu, Real Madrid tisa

NAMBA Pict

Muktasari:

  • Mabao yamekuwa yakifungwa kwa wingi katika ligi bora za Ulaya, lakini ni timu zipi ambazo zimekuwa hatari zaidi mbele ya lango hadi sasa?

ZURICH, USWISI: TIMU 20 zenye mashambulizi makali zaidi Ulaya msimu huu zimetajwa, lakini ndani yake kuna maajabu kama siyo mishangao! Real Madrid imeshika nafasi ya tisa, huku Brighton inayokipiga katika Ligi Kuu England ikikamata namba tatu; kulikoni?

Mabao yamekuwa yakifungwa kwa wingi katika ligi bora za Ulaya, lakini ni timu zipi ambazo zimekuwa hatari zaidi mbele ya lango hadi sasa?

Msimu bado uko katika hatua za mwanzo huku kukiwa na mapumziko ya wiki tatu kwa ajili ya mechi za kimataifa. Hata hivyo, baadhi ya timu kubwa Ulaya tayari zimeonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao, ilhali zipo ambazo hazikutegemewa sana nazo zikifanya vizuri.

Transfermarkt imetumia wastani wa mabao kwa kila mchezo (GPG) kupima ubora wa safu za ushambuliaji za timu katika ligi tano za Ulaya; Engalnd (EPL), Hispania (LaLiga), Italia (Serie A), Ujerumani (Bundesliga) na Ufaransa (Ligue 1).

Katika suala la mabao Transfermarkt imeeleza kuwa Bundesliga ndiyo iliyotoa timu nyingi zaidi katika 20 bora, ikiwa nazo saba. Kwa upande mwingine, Ligue 1 ina timu mbili ndani ya 20 bora.

Orodha hiyo imetengenezwa kwa kuangalia wastani wa mabao kwa kila mchezo, hivyo haiwakilishi moja kwa moja idadi kubwa zaidi ya mabao yaliyofungwa kwa jumla; idadi ya mechi ambazo kila timu imecheza pia inazingatiwa. Hii ndiyo 10 bora ya timu hizo.

Kinara wa orodha hiyo ni Barcelona, ambayo imekuwa ikifunga kwa wingi wa mabao chini ya kocha Hansi Flick, ambapo imeshinda michezo yote saba ya mwanzo ya LaLiga, huku ikifunga mabao 31.

NAMB 01

Mshambuliaji Raphinha amechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo akiwa tayari amefunga mabao 12. Hiyo inaipa Barcelona wastani wa mabao 4.43 kwa kila mchezo, na kuiweka kileleni mwa timu zote 20.

Bayern Munich inashika nafasi ya pili ikiwa na wastani wa mabao 3.50 kwa mchezo katika mechi zake nne za mwanzo za Bundesliga.

Mpaka sasa licha ya kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, timu imefunga mabao manne.

Kinachoshangaza ni kwamba Brighton imeingia nafasi ya tatu baada ya kuanza vizuri msimu wa Ligi Kuu England ikifunga wastani wa mabao 3.20 kwa mchezo katika mechi zake tano za kwanza ikiwa tayari imeshaingia kambani mara 16 zaidi ya vinara wa ligi hiyo, Manchester City waliofunga mara 13.

NAMB 02

Freiburg (Bundesliga) na Inter Milan (Serie A) zinakamilisha tano bora, kila moja ikiwa na wastani wa mabao 3.00 kwa mchezo. Inter Milan imeingia kambani mara 15 katika mechi tano ikikamata nafasi ya pili nyuma ya AS Roma kwenye msimamo. Kwa Freiburg, imefunga mabao 12 katika mechi nne.

AS Roma (Serie A) inakamata nafasi ya sita kwa wastani wa 2.80 GPG ikiwa imetupia mabao 14 katika mechi tano, huku Augsburg ya Bundesliga inashika nafasi ya saba ikiwa na wastani wa mabao 2.75 ikiingia kambani mara 11 katika mechi nne, ilhali vinara wa England, Manchester City, wakiwa nafasi ya nane kwa wastani wa mabao 2.60 wakiwa nayo 13 hadi sasa.

Real Madrid inashika nafasi ya tisa ikiwa na wastani wa mabao 2.57 ikiwa imefunga mara 18 katika mechi saba, huku Bayer Leverkusen ikikamilisha timu 10 bora ikiwa na wastani wa kufunga mabao 2.50 ikifunga orodha hiyo kwa kufunga mara 10 katika mechi nne.