Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yapata pigo, Tzolis aumia

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Tzolis, mwenye umri wa miaka 24, alianza katika kikosi cha Ugiriki kwenye mchezo huo uliokuwa na umuhimu mkubwa, lakini alidumu uwanjani kwa dakika 18 pekee kabla ya kutolewa kutokana na majeraha.

SALONIKA, UGIRIKI: ARSENAL imepata hofu baada ya winga wake  kuumia wakati akiitumikia timu ya taifa ya Ugiriki katika mchezo wa Ligi ya Mataifa dhidi ya Uholanzi.

Tzolis, mwenye umri wa miaka 24, alianza katika kikosi cha Ugiriki kwenye mchezo huo uliokuwa na umuhimu mkubwa, lakini alidumu uwanjani kwa dakika 18 pekee kabla ya kutolewa kutokana na majeraha.

Winga huyo alianza vizuri na alikaribia kuifungia Ugiriki bao dakika ya 13, lakini bao hilo lilikataliwa baada ya Vangelis Pavlidis wa Benfica kuonekana kuingilia mchezo akiwa katika nafasi ya kuotea.

Dakika tano baadaye, Tzolis alianguka uwanjani akionekana kushikilia sehemu ya nyuma ya paja lake la kulia.

ARSEN 01

Madaktari wa timu hiyo walimfanyia vipimo uwanjani huku mchezaji huyo akionekana kuvunjika moyo, akifunika uso wake kwa mikono yote miwili.

Kocha wa Ugiriki, Ivan Jovanovic, hakuchukua muda na kumtoa Tzolis, nafasi yake ikichukuliwa na Giorgos Masouras.

Tzolis alikuwa akimpa wakati mgumu beki wa kulia wa Real Madrid, Denzel Dumfries, katika upande wa kushoto wa mashambulizi ya Ugiriki kabla ya kuonekana kuvuta misuli ya mguu wa kulia.

Jeraha hilo limeongeza wasiwasi Arsenal, hasa kutokana na Tzolis kuanza kwa kiwango kizuri msimu huu wa Ligi Kuu England tangu alipohamia klabuni hapo akitokea Club Brugge kwa ada ya rekodi ya pauni35 milioni.

Tzolis ameumia wakati ambapo Arsenal tayari imepata changamoto kadhaa za majeraha katika kipindi hiki cha mapumziko ya mechi za kimataifa.

ARSEN 02

Kai Havertz, Martin Odegaard na Ezri Konsa wamepata majeraha, huku Declan Rice na Piero Hincapie wakijiondoa kwenye vikosi vya mataifa yao kutokana na matatizo ya kiafya.

Hata hivyo, kuna jambo la kumtia moyo kocha Mikel Arteta baada ya Tzolis kubaki kwenye benchi la Ugiriki badala ya kwenda moja kwa moja chumba cha matibabu.

Mchezaji huyo alionekana akiwa ameketi pamoja na wachezaji wa akiba na baadaye kushangilia mabao yote mawili ya Ugiriki katika kipindi cha kwanza.

Masouras, aliyeingia kuchukua nafasi yake, alihusika katika bao la kwanza lililofungwa na Fotis Ioannidis, kabla ya yeye mwenyewe kufunga bao la pili wakati wa nyongeza.

Taarifa zinaeleza kuwa Tzolis atafanyiwa tathmini Ijumaa ili kubaini kama amevuta au kuchanika misuli ya nyuma ya paja.