Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benjamin Sesko aipa sharti moja Arsenal amwage wino

TETESI Pict

Muktasari:

  • Sesko ambaye amekuwa katika rada za Arsenal tangu kuanza kwa dirisha hili la usajili ameripotiwa kufikia makubaliano binafsi na Arsenal na yupo tayari kujiunga nayo.

STRAIKA wa RB Leipzigz, Benjamin Sesko ameipa Arsenal sharti la kuweka kipengele maalumu kwenye mkataba wake ambacho kitakuwa kinaeleza ni kiasi gani kikilipwa na timu itakayomhitaji anaweza kuondoka katika kikosi hicho.

Sesko ambaye amekuwa katika rada za Arsenal tangu kuanza kwa dirisha hili la usajili ameripotiwa kufikia makubaliano binafsi na Arsenal na yupo tayari kujiunga nayo.

Mabosi wa timu hiyo kwa sasa wanapambana kuhakikisha kwamba wanamalizia mazungumzo na RB Leipzig kwa ajili ya kukubaliana masuala ya ada ya uhamisho.

Utaratibu wa kuwepo kipengele cha kumruhusu mchezaji kuondoka ikiwa pesa husika zitalipwa haujazoeleka sana England, lakini Sesko ametoa maelekezo hayo na inaelezwa vigogo wa Arsenal wamekubaliana nayo. Nyota huyo anasajiliwa na Washika Mitutu kwa ajili ya kuboresha safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa na upungufu.


Joao Palhinha

MANCHESTER United inasubiri kuona kama Bayern Munich itakubali ombi la kutaka kumsajili kiungo Joao Palhinha kutoka kwa wababe hao wa Ujerumani kwa mkopo wa msimu mmoja.

Man United imefikia uamuzi wa kutuma maombi ya kumsajili Palhinha kwa mkopo baada ya kuona uwezekano wa kuipata saini ya kiungo wa Atalanta, Ederson ni mdogo kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kinachohitajika na timu yake.


Marc Guehi

LIVERPOOL ni kati ya timu zilizoingia katika vita ya kuiwania saini ya beki wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi, 24, katika dirisha hili.

Beki huyu ambaye alionyesha kiwango bora akiwa na England kwenye michuano ya Euro mwaka jana na mechi mbalimbali akiwa na Palace, yupo tayari kuondoka lakini hatma yake ameiacha mikononi mwa Palace ambayo bado ina mkataba naye.


Illia Zabarni

MABOSI wa Bournemouth wapo tayari kumuuza beki wao wa kati raia wa Ukraine, Illia Zabarni katika dirisha hili la majira ya kiangazi ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 59 milioni.  Zabarni mwenye umri wa miaka 22, amezivutia timu nyingi kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa na Bournemouth msimu uliomalizika na PSG inadaiwa kuwa imeshaanza hadi mazungumzo kwa ajili ya kumsajili.


Mohammed Kudus

NEWCASTLE United inatarajiwa kuwasilisha ofa rasmi kwenda West Ham baada ya mazungumzo yao na wawakilishi wa winga wa West Ham, Mohammed Kudus, 24, kwenda vizuri.

Mabosi wa Newcastle wameangukia kwa Kudus baada ya kushindwa kuipata saini ya straika wa Brentford, Bryan Mbeumo anayeonekana kuwa karibu zaidi kujiunga na Manchester United ambayo imeshafanya naye makubaliano binafsi.


Maxime Esteve

BURNLEY imeendelea kushikilia msimamo wa kuhitaji Pauni 50 milioni ili kumuuza beki wake wa kati raia wa Ufaransa, Maxime Esteve, 23, ambaye anawindwa sana na  Bayern Munich.

Inaelezwa kocha wa Bayern, Vincent Kompany ni shabiki mkubwa wa staa huyu ambaye aliwahi kumfundisha akiwa katika kikosi cha Burnley.


Dayot Upamecano

MAZUNGUMZO kati ya wawakilishi wa Bayern Munich na beki wao wa kimataifa wa Ufaransa, Dayot Upamecano, 26, juu ya mkataba mpya yamesimama kwa muda na yanatarajiwa kumalizika baada ya wababe hao wa Ujerumani kumaliza ushiriki wao kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la klabu. Upamecano ni miongoni mwa nyota tegemeo kikosini Bayern.


Nuno Tavares

LAZIO imefikia hatua nzuri katika mazungumzo yake na Arsenal juu ya kumsainisha mkataba wa kudumu beki wa kushoto, Nuno Tavares katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Mabosi wa Lazio wanataka kutoa kiasi hicho cha pesa baada ya ripoti ya kocha wao kusisitiza kwamba asajiliwe kwani ameridhishwa na kiwango alichoonyesha msimu uliopita.