Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bei ya Semenyo yashtua vigogo wa soka England

Muktasari:

  • Yanga yaendelea kutamba kumfunga Simba, yaweka bango Zanzibar

MANCHESTER United, Newcastle na Tottenham zote zimeonyesha kukatia tamaa uwezekano wa kuipata saini ya mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya wa Ghana, Antoine Semenyo, mwenye umri wa miaka 25.

Ripoti zinaeleza Bournemouth inahitaji Pauni 70 milioni ili kumuuza staa huyu.

Timu nyingi ambazo zinamhitaji Semenyo zimeishia kwenye Pauni 60 milioni na nyingine Pauni 50 milioni.

Vigogo wamevutiwa sana na fundi huyu kutokana na kiwango bora alichoonyesha kwa msimu uliopita ambapo alicheza mechi 42 za michuano yote, amefunga mabao 13 na kutoa asisti saba.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Bryan Mbeumo

MSHAMBULIAJI wa Brentford na timu ya taifa ya Cameroon, Bryan Mbeumo, mwenye umri wa miaka 25, ameziambia Brentford na Tottenham kuwa uamuzi wake ni kwamba atajiunga na Manchester United iwapo ataondoka katika dirisha hili la majira ya kiangzi.

Kumekuwa na mazungumzo baina ya mabosi wa Brentford na wawakilishi wa staa huyu wakimshawishi abakie, pia Tottenham nayo inahitaji kumsajili lakini Mbeumo ameshafanya uamuzi wa kujiunga na Man United.


Jarrad Branthwaite

BEKI wa kati wa Everton na timu ya taifa ya England, Jarrad Branthwaite, mwenye umri wa miaka 23, yuko tayari kusaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kusalia kwenye timu hiyo licha ya kuhusishwa na timu mbalimbali kubwa barani Ulaya.

Mbali ya Jarrad mabosi wa Everton pia wana matumaini kuwa kiungo wao wa kati wa kimataifa wa Senegal Idrissa Gueye, mwenye umri wa miaka 35, atasaini mkataba mpya wa mwaka mmoja.


Harvey Elliott

RB Leipzig, ni kati ya timu zilizoingia kwenye vita ya kuiwania saini ya kiungo wa Liverpool na England, Havery Elliott hivi karibuni baada ya kuelezwa kuwa huenda akaondoka katika dirisha hili.

Elliott mwenye umri wa miaka 22, anataka kuondoka ili kujiunga na timu itakayompa nafasi ya kucheza na mbali ya Leipzig, Brighton na West Ham zilitajwa hapo awali kuwa zinamhitaji.


Douglas Luiz

LEEDS United imeanza mazungumzo ya awali na Juventus kuhusu kiungo wa kati wa Brazil, Douglas Luiz, mwenye umri wa miaka 27, inayehitaji kumsajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Leeds ambayo imepanda daraja kucheza Ligi Kuu England msimu ujao inataka kusuka upya kikosi chake kwa kuwa na wachezaji wenye uzoefu ambao watasaidia kufanya vizuri katika EPL msimu ujao.


Timothy Weah

NOTTINGHAM Forest imeachana na mpango wa  kumsajili winga wa Juventus mwenye umri wa miaka 25, Timothy Weah, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani kukataa ofa yao.  Forest ilikuwa imekubaliana kutoa ada ya karibu Pauni 19 milioni pamoja na winga Mbelgiji Samuel Mbangula, mwenye umri wa miaka 21 kama sehemu ya ofa ili kumpata Weah.


Neil El Aynaoui

ASTON Villa inakabiliana na ushindani kutoka kwa timu mbili za Italia ambazo ni Juventus na Lazio juu ya mpango wa kutaka kumsajili   kiungo wa kati wa Lens, Neil El Aynaoui, ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Morocco chini ya miaka 23.

Villa imetuma wawakilishi wake kwenda Ufaransa kufanya mazungumzo na Lens.


Eberechi Eze

MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace, Eberechi Eze, ni miongoni mwa wachezaji ambao Arsenal inahitaji kuwasajili katika dirisha hili lakini wanakumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa Tottenham. Mchezaji huyu  wa kimataifa wa England  (26) yeye pia amewaambia mabosi wa Palace kuwa anahitaji kuondoka kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.