Barcelona yarejea Camp Nou, kuanza na Athletic Club
Muktasari:
- FC Barcelona imetoa taarifa jioni hii ya leo Jumatatu kuthibitisha kuwa mechi yao ijayo ya La Liga dhidi ya Athletic Club iotapigwa kwenye uwanja huo siku ya Jumamosi.
BARCELONA, HISPANIA: KLABU ya Barcelona inatarajiwa kurejea tena kucheza kwenye Uwanja wa Camp Nou.
FC Barcelona imetoa taarifa jioni hii ya leo Jumatatu kuthibitisha kuwa mechi yao ijayo ya La Liga dhidi ya Athletic Club iotapigwa kwenye uwanja huo siku ya Jumamosi.
Hatimaye Barcelona inarejea Camp Nou baada ya kutumia miezi mingi Montjuïc na hata kucheza mechi mbili kwenye uwanja mdogo wa Johan-Cruyff msimu huu.
Lakini sasa imetangaza rasmi kuwa, mechi ujao wa La Liga utakapigwa Jumamosi kuanzia saa 10 jioni utapigwa kwenye uwanja huo maarufu wenye uwezo wa watazamaji 45,401.
Hii inafuatia 'kupata kibali cha kwanza cha matumizi kwa awamu ya 1B.”
Kazi ya ukarabati inaendelea kwenye uwanja huo, lakini Barcelona ilipokea leseni kutoka kwa Halmashauri ya eneo hilo leo Jumatatu inayowaruhusu kuandaa mechi kwa uwezo wa juu uliowekwa wa watazamaji na kwamba tiketi zimeanza kuuzwa kuanzia leo hii.
Aidha, klabu imesema inafanya kazi kukamilisha uthibitisho wa Awamu ya 1C “ili kuhakikisha ufunguzi wa upya wa Gol Nord, kwa kutimiza mahitaji yote ya uendeshaji, usalama na faraja kwa wanachama na mashabiki.”
Hatimaye, Barcelona inatarajia kupata idhini ya UEFA kuandaa mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani iliyopangwa kuchezwa Desemba 9.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, masharti yote ya awali yametimizwa na kinachosubiriwa sasa ni uthibitisho wa mwisho tu.
Kazi ya ukarabati inaendelea kwenye uwanja huo, lakini Barcelona ilipokea leseni kutoka kwa halmashauri ya eneo hilo siku ya Jumatatu inayowaruhusu kuandaa mechi kwa uwezo wa juu uliowekwa wa watazamaji