Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona yampigia hesabu Harry Kane atue Catalonia

TETESI Pict

Muktasari:

  • Mabosi wa Barcelona wanataka saini ya Kane ili akawe mbadala wa Robert Lewandowski, 37,  anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

BARCELONA inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na nahodha wa timu ya taifa ya England  Harry Kane, 32, ambaye hadi sasa amefunga mabao 95 katika mechi 102 za michuano yote tangu ajiunge na timu hiyo.

Mabosi wa Barcelona wanataka saini ya Kane ili akawe mbadala wa Robert Lewandowski, 37,  anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Kane ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, hajasema jambo lolote kuhusu tetesi hizo.

Barcelona inataka kuhakikisha inakuwa na mshambuliaji mwenye uzoefu na inaamini haitotoa kiasi kikubwa cha pesa kukamilisha uhamisho wake kutokana na umri alionao.

Tangu kuanza kwa msimu huu Kane ambaye alitua Bayern mwaka 2023 kwa dau la Euro 95 milioni amecheza mechi 11, amefunga mabao 13 na kutoa asisti nne.


Eduardo Camavinga

CHELSEA, Manchester United na Newcastle United zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Eduardo Camavinga, 22, dirisha lijalo la majira ya baridi. Camavinga ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja kiwanjani lakini amekuwa akisumbuliwa sana na majeraha ya mara kwa mara yanayosababisha muda mwingi awe nje ya Uwanja. Real Madrid ilimsajili Camavinga kutoka Rennes kwa Euro 31 milioni  mwaka  2021.


Elliot Anderson

KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, ameahidiwa kupewa fungu kwa ajili ya kufanya usajili wa kiungo wa Nottingham Forest na England, Elliot Anderson, 22, katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Anderson, ambaye alijiunga na Nottingham Forest mwaka 2021 kutoka Newcastle United, ameonyesha kiwango bora tangu msimu uliopita na Amorim anahitaji saini yake kabla ya kumruhusu Casemiro kuondoka.


Ryan Gravenberch

REAL Madrid imeonyesha nia ya kumsajili kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Ryan Gravenberch, 23, ifikapo mwisho wa msimu huu.  Gravenberch ambaye amefunga bao moja kati mechi nne za michuano yote msimu huu, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Madrid inamwona Gravenberch kama mbadala wa muda mrefu wa Eduardo Camavinga ambaye huenda akaondoka dirisha lijalo Januari.


William Saliba

ARSENAL ina imani beki wao kisiki wa timu ya taifa ya Ufaransa, William Saliba, 24, atasaini mkataba mpya wa muda mrefu licha ya kuhitajika na Real Madrid. Mkataba wa Saliba unatarajiwa mwaka 2027,  na sas Arsenal inataka kumpa mkataba mpya wa miaka mitano utakaokuwa na ongezeko la mshahara. Mkataba huo mpya unatakuwa unamalizika mwaka 2029.


Jack Grealish

Everton ina matumaini makubwa ya kumsainisha mkataba wa moja kwa moja staa wa Manchester City, Jack Grealish kwa pesa dau la chini tofauti na kipengele ambacho kimewekwa. Katika mkataba wa makubaliano ya kumtoa kwa mkopo kwenda Everton, Man City iliweka kipengele kinachoitaka timu hiyo kulipa Pauni 50 milioni ili kumsainisha mkataba wa kudumu.


Jeremy Monga

REAL Madrid imetuma skauti England ili kumtazama winga chipukizi wa Leicester City, Jeremy Monga,16, anayechezea kikosi cha vijana cha  England U19. Monga ni miongoni mwa wachezaji wenye kasi na uwezo wa kumiliki mpira. Pia amekuwa akilinganishwa na Jadon Sancho katika mbinu zake za  kiuchezaji.


Luis Benedetti

NAPOLI ndiyo inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuipata saini ya beki wa kati wa Palmeiras, Luiz Gustavo Benedetti, 19. Fundi huyu wa kimataifa wa Brazil ni moja ya vipaji vinavyoibukia nchini humo msimu uliopita na timu hiyo inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 30 milioni ili kumuuza. Mkatanba wa sasa wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.