Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao moja la Neymar Saudia  lanunua viwanja 13 vya Mkapa

Muktasari:

  • Staa huyo wa Kibrazili alivunjiwa mkataba huko Al-Hilal baada ya kuichezea timu hiyo kwa miezi 18.

LONDON, ENGLAND: NDO hivyo. Supastaa Neymar ameishtua dunia ya mchezo wa soka kwa maisha yake ya huko Saudi Arabia kwamba aliiuzia timu ya Al Hilal bao moja kwa zaidi ya Pauni 200 milioni baada ya kufunga mara moja katika mechi saba alizocheza.

Staa huyo wa Kibrazili alivunjiwa mkataba huko Al-Hilal baada ya kuichezea timu hiyo kwa miezi 18.

Neymar, 32, aliumia misuli ya goti baada ya kuichezea Al Hilal mechi tano, Oktoba 2023. Na aliporejea uwanjani mwaka mmoja baadaye, Mbrazili huyo aliumia tena na kurudi kwenye chumba cha wagonjwa - safari hii akisumbuliwa na misuli ya paja.

Neymar kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho za kurudi kwenye klabu yake ya utotoni, Santos ya Brazil baada ya Al Hilal kuamua kuachana naye. Licha ya kushindwa kufanya vizuri huko Saudia, fowadi huyo anarudi kwao Brazil akaunti yake ya benki ikiwa imejaa pesa.

Neymar alisaini mkataba wa miaka miwili Al-Hilal wakati alipotua kwenye timu hiyo kwa ada ya Pauni 78 milioni akitokea Paris Saint-Germain mwaka 2023. Na klabu hiyo ilikubali kumlipa Neymar mshahara wa Pauni 129.2 milioni kwa mwaka.
Na baada ya kuondoka kwenye timu hiyo baada ya miezi 18, hiyo ina maana alivuna Pauni 193.8 milioni.

Hiyo ni sawa na mchanganuo wa Pauni 2.5 milioni kwa wiki. Ukiunganisha na ada yake ya uhamisho, hiyo ina maana Al-Hilal ilitumia Pauni 271 milioni (sawa na fedha za Kitanzania Sh853 bilioni) kununua bao moja tu la Neymar, huku mechi zake saba alizocheza kila moja iliigharimu timu hiyo Pauni 38.7 milioni. 

Ina maana pesa ambayo Al Hilal imelipa kwenye bao moja la Neymar sawa na kujenga viwanja vya soka 13 vya ubora ule wa Mkapa ulipo Dar es Salaam. Uwanja wa soka wa Mkapa unaripotiwa kugharimu zaidi ya Sh56 bilioni kwenye ujenzi wake.

Neymar bado atalipwa Pauni 51.9 milioni ikiwa ni malipo ya sehemu iliyobaki ya msimu, ambapo amekubali kupunguza asilimia 15 tu, ambayo ni Pauni 8 milioni. Hiyo ina maana hadi mwisho wa msimu, kwa bao moja alilofunga kwenye timu hiyo itakuwa imelipia Pauni 322 milioni, huku kila mechi moja atakuwa ameigharimu Pauni 46 milioni.

Kama hiyo haitoshi, Neymar alivuna pia Pauni 136 milioni kwenye bili za matangazo ya biashara - hiyo ni nje ya mshahara wa Al-Hilal. 

Uamuzi wa kumtema Neymar umekuja baada ya kocha Jorge Jesus kukiri kwamba mchezaji huyo hawezi tena kuendelea na nguvu inayohitajika kwenye timu.

Kocha Jesus amesema: “Neymar hawezi tena kucheza kwenye viwango tunavyovitaka. Mambo yamekuwa magumu kwake kwa bahati mbaya.”

Neymar ametambua kushindwa kucheza na baada ya taarifa ya klabu, akasema: "Kwa kila mtu wa Al Hilal, mashabiki, asanteni!!!!"


NEYMAR NA MAMBO YA PESA DAMDAM 


Wakati Neymar anahama kutoka Barcelona kwenda Paris Saint-Germain mwaka 2017, saini yake iligharimu Pauni 198 milioni -  ada ambayo iliweka rekodi ya dunia kwenye uhamisho. Kwa mujibu wa Footmercato, Neymar alivuna hadi Euro 36 milioni kwa mwaka kwenye dili lake PSG.

Hiyo ina maana kwamba kwa muda huo aliokuwa Paris, huduma yake iligharimu Euro 3 milioni kwa mwezi, Euro 700,000 kwa wiki au Euro 100,000 kwa siku. Tofauti na alivyokuwa kwenye timu nyingine kuanzia Santos, Barcelona na PSG, supastaa Neymar ameipunja sana Al Hilal licha ya kumlipa kibosi.

Ukiweka kando bao lake moja alilofunga akiwa na kikosi hicho cha Saudi Pro League, kingine alichofanya ni asisti tatu tu. Miezi 18 amecheza mechi saba.

Neymar ana uwezo wa kucheza kwenye mstari wote wa safu ya ushambuliaji - iwe kushoto, kulia au kati alifunga mabao 136 na asisti 64 katika mechi 225 alipokuwa kwenye kikosi cha Santos. Alihamia Barcelona mwaka 2013 ambako alifunga mabao 105 na asisti 76 katika mechi 186 na kushinda La Liga mara mbili na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mmoja kwenye kipindi cha miaka minne katika kikosi hicho cha Nou Camp.

Kwenye kikosi cha PSG alifunga mabao 118 na asisti 77 katika mechi 173. Hiyo ina maana alihusika kwenye mabao 195 katika mechi 173, ambayo ni huduma bora kabisa. Akiwa Barca alihusika kwenye mabao 181 katika mechi 186.