Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la Olise lampagawisha Zidane

OLISE Pict

Muktasari:

  • Zidane, ambaye alichukua mikoba ya Ufaransa baada ya kuondoka kwa Didier Deschamps, ameanza safari yake kwenye benchi la Les Bleus kwa kishindo, akishinda mechi zote mbili alizosimamia hadi sasa.

PARIS, UFARANSA: KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Ufaransa, Zinedine Zidane, amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kushindwa kujizuia kwa furaha kufuatia timu yake kupata ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Ubelgiji.

Zidane, ambaye alichukua mikoba ya Ufaransa baada ya kuondoka kwa Didier Deschamps, ameanza safari yake kwenye benchi la Les Bleus kwa kishindo, akishinda mechi zote mbili alizosimamia hadi sasa.

Baada ya kuiongoza Ufaransa kuifunga Uturuki 1-0 katika Ligi ya Mataifa Ijumaa iliyopita, Zidane alirudia matokeo hayo hayo jana Jumatatu, safari hii Ubelgiji ikiwa mwathirika.

Shujaa wa ushindi huo alikuwa winga wa Bayern Munich, Michael Olise, aliyefunga bao pekee dakika ya 88 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.

Bao hilo lilipopatikana, Zidane naye akasahau kabisa kwamba alikuwa kocha.

Dakika hiyo hiyo mpira ulipoingia wavuni, kocha huyo mwenye umri wa miaka 54 alikimbia pembeni mwa uwanja kwa furaha, akishangilia kama mchezaji aliyefunga bao la ushindi.

Lakini hakutosheka. Zidane alichukua mpira mwingine uliokuwa umewekwa pembeni mwa uwanja juu ya koni, kisha akaupiga kwa nguvu kwa furaha, ukapaa huku benchi la Ufaransa likiruka kwa shangwe nyuma yake.

Kitendo hicho kimezua gumzo mitandaoni, huku video na picha za Zidane zikisambaa na kumfanya kuwa ‘meme’ wa siku.

OLI 01

Zidane, aliyestaafu kucheza mwaka 2006, sasa amerejea kwenye usimamizi baada ya kuondoka Real Madrid mwaka 2021.

Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka minne kuinoa Ufaransa, akichukua nafasi ya Deschamps ambaye aliiongoza timu hiyo kwa miaka 14.

Deschamps alimaliza utawala wake baada ya Kombe la Dunia, ambako Ufaransa ilifungwa 2-0 na Hispania katika nusu fainali na baadaye kumaliza nafasi ya nne baada ya kufungwa 6-4 na England katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.

Kwa Zidane, hii ni nafasi aliyokuwa akiisubiri kwa muda mrefu.

Wakati akizinduliwa kama kocha wa Ufaransa, alisema timu hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yake kubwa baada ya kuondoka Real Madrid.

Zidane alisema hakutaka kuchukua kazi nyingine ya ukocha kwa sababu alitaka kusubiri nafasi ya kuinoa nchi yake.

“Timu ya taifa ya Ufaransa ndiyo kitu pekee nilichokuwa nataka kufanya,” alisema Zidane.

Aliongeza kuwa muda wote alikuwa akiitazama timu hiyo kwa jicho la kocha wa baadaye na kwamba baada ya Deschamps kutangaza kuondoka, alijua mara moja kuwa alitaka kuchukua nafasi hiyo.

Deschamps ameacha historia kubwa Ufaransa, akisimamia michezo 185 na kushinda 120.

Chini yake, Ufaransa ilitwaa Kombe la Dunia 2018, Ligi ya Mataifa msimu wa 2020/21, huku pia ikifika fainali za Euro 2016 na Kombe la Dunia 2022.

OLI 02

Cha kuvutia zaidi, Deschamps na Zidane si wageni. Wawili hao walikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 1998, kwenye ardhi ya nyumbani.

Zidane alikuwa mmoja wa mastaa wakuu wa mafanikio hayo, huku mwaka huo huo akitwaa tuzo ya Ballon d’Or.

Akiwa na Ufaransa, Zidane alicheza mechi 108, akifunga mabao 31 na kutoa pasi 29 za mwisho.

Ufaransa bado ina mechi mbili katika mapumziko haya ya kimataifa. Ijumaa itakutana na Italia, kabla ya kurudiana na Ubelgiji Jumatatu ijayo.