Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta azima uvumi wa Gyokeres kuondoka Arsenal

Muktasari:

  • Katika siku za hivi karibuni, taarifa mbalimbali zilidai kuwa Gyokeres angeweza kutumika kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wachezaji ili Arsenal impate mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amevunja ukimya kuhusu hatma ya mshambuliaji Viktor Gyokeres kwa kusisitiza kuwa nyota huyo hatauzwa katika dirisha hili la usajili, licha ya kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Hispania.

Katika siku za hivi karibuni, taarifa mbalimbali zilidai kuwa Gyokeres angeweza kutumika kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wachezaji ili Arsenal impate mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.

Hata hivyo, Arteta amekanusha uvumi huo na kuweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden bado ni sehemu muhimu ya mipango yake.

"Atabaki hapa," alisema Arteta kwa ufupi alipoulizwa kuhusu mustakabali wa Gyokeres.

Gyokeres, aliyesajiliwa kwa ada ya pauni milioni 63.5 (takribani Sh226.11 bilioni), alikuwa mfungaji bora wa Arsenal msimu uliopita na amekuwa mmoja wa nyota wanaotegemewa na mabingwa hao wa Ligi Kuu England.

Kuhusu taarifa zinazomhusisha Julian Alvarez kuhamia Emirates, Arteta alikataa kuzungumzia uvumi huo, akisema si sahihi kutoa maoni kuhusu mchezaji ambaye bado yupo chini ya mkataba na klabu nyingine.

"Siwezi kuzungumzia mchezaji wa klabu nyingine," alisema Arteta.

Kauli hiyo imeweka wazi msimamo wa Arsenal kwamba Gyokeres ataendelea kuiongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuelekea msimu mpya, huku tetesi za kuondoka kwake zikionekana kupoteza nguvu.