Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta aponzwa na kauli yake, mashabiki wamvaa

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Arsenal itakwenda Old Trafford kumenyana na Manchester United kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England, leo Jumapili, ikijaribu kukwepa anguko jingine la kutoka kapa msimu huu.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amekosolewa na mashabiki baada ya kutoa namba ambazo zinakinzana na ukweli mbele ya waandishi wa habari.

Arsenal itakwenda Old Trafford kumenyana na Manchester United kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England, leo Jumapili, ikijaribu kukwepa anguko jingine la kutoka kapa msimu huu.

Baada ya misimu mitatu ya kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi, ikizidiwa mara mbili na Manchester City na moja dhidi ya Liverpool, kocha Arteta anaamini kikosi chake kikiendelea kucheza kwa kiwango cha sasa kitabeba ubingwa.

Arteta alisema: “Unachimba, unachimba, unachimba, utaendelea kuchimba na siku moja utapata dhahabu. Hivyo ndivyo ilivyo mara zote. Unapojifunza, basi utaelimika, ipo hivyo.”

Arteta, 43, aliongeza: “Kwa misimu mitatu yimekusanya pointi nyingi kuliko timu nyingine yoyote kwenye ligi hii, hiyo ni safi. Hilo linaonyesha jinsi ulivyolinda kiwango kwa muda wote. Na sasa, tunataka kulifanya hilo kwenye msimu huu, kukusanya pointi moja zaidi ya za wengine au kufunga mabao mengi zaidi ya wengine. Hayo ndiyo malengo.”

Hata hivyo, wakati Arteta akibainisha hilo na mipango yake ya Emirates, namba za timu hiyo si nyingi kama madai ya Mhispaniola huyo. Kwa misimu mitatu iliyopita, Arsenal imekusanya pointi 247: 84 msimu wa 2022/23, 89 msimu wa 2023/24 na 74 kwenye msimu wa 2024/25.

Namba hizo si mbaya, lakini bado Arteta alishindwa mbele ya bosi wake wa zamani, Pep Guardiola, anayekinoa kikosi cha Man City.

Wakati Arsenal ikiwa kwenye kiwango bora kabisa, Man City imeshinda mataji mawili msimu wa 2020/21 na 2023/24. Ndani ya misimu hiyo mitatu, wakati Man City inabeba ubingwa kwa kuvuna pointi 89 na 91 na msimu uliopita, iliposhika nafasi ya tatu, ilivuna pointi 71. Lakini, kwa ujumla, Man City imevuna pointi 251 katika kipindi hicho cha misimu mitatu.

Wakati huo, mabingwa watetezi Liverpool imevuna pointi 233 katika misimu mitatu ya mwisho: 67 katika msimu wa 2022/23, 82 msimu wa 2023/24 na 84 katika msimu wa 2024/25. Pamoja na pointi zao chache, lakini Liverpool imebeba ubingwa, wakati Arsenal haijachukua taji lolote na pointi zao nyingi.

Shabiki mmoja alisema: “Namba hazipo sawa, kwa misimu mitatu iliyopita, Man City imevuna pointi 251, Arsenal 247, Liverpool 233. Arsenal ya pili tena.”

Shabiki wa pili alisema: “Misimu mitatu tumevuna pointi nyingi kuliko timu nyingine kwenye ligi, taji lipo wapi?”

Shabiki wa tatu aliongeza: “Wanapaswa kuacha kuchimba, wacheze mpira.”

Na shabiki mwingine alisema: “Hii inamfanyaje kuwa na ujasiri. Timu yenye pointi nyingi kwa msimu ndiyo inayoshika ubingwa wa Ligi Kuu England na sio pointi za jumla za miaka kibao. Huu ni wakati wa Arsenal kuachana na huyu mtu kwa sababu ameshapoteza.”

Shabiki wa tano alisema: “Arteta ni kama anatoa maongezi ya vichekesho tu badala ya kuzungumza na waandishi juu ya mbio za ubingwa.”

Kwa kauli hiyo ya Arteta, imefanya kufanyika kwa kutazama klabu nyingine za Ligi Kuu England zimevuna pointi kiasi gani katika kipindi cha misimu mitatu.

Inayokamilisha nafasi ya nne katika pointi za jumla ni Newcastle United ikiwa imekusanya pointi 197, huku Aston Villa ikishika namba tano kwa pointi 195. Licha ya kufanya hovyo msimu uliopita, Man United imeshika namba sita kwenye pointi za misimu mitatu ilipovuna 177. Hiyo ni pointi moja zaidi ya ilizovuna Chelsea, ambayo imetumia mamilioni ya pesa kujaribu kushinda taji hilo la Ligi Kuu England. Brighton yenyewe imekusanya pointi 171. Tottenham inafuatia ikiwa na pointi 164. Brentford ilishuka kiwango chake misimu miwili iliyopita baada ya kupoteza mastaa wao wenye majina makubwa kama Ivan Toney, lakini bado imevuna pointi 154.