Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yafanya umafia London

UMAFIA Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta, pamoja na Kocha Mikel Arteta, walikutana na Eberechi Eze mwezi uliopita na mchezaji huyo alishawishika kuhamia Emirates, lakini wakati huo ofa rasmi haikuwasilishwa kwa Palace.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imefanya umafia wa kuipokonya tonge mdomoni Tottenham Hotspurs kwa kuingilia dili lao la kiungo mshambuliaji wa Crystal Palace, Eberechi Eze dirisha hili.

Inaelezwa Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta, pamoja na Kocha Mikel Arteta, walikutana na Eberechi Eze mwezi uliopita na mchezaji huyo alishawishika kuhamia Emirates, lakini wakati huo ofa rasmi haikuwasilishwa kwa Palace.

Baada ya Arsenal kutoonyesha nia ya kuendelea hapo awali, Spurs iliingilia kati na kuanza mazungumzo na Palace na inadaiwa yalifikia mwafaka juzi, Jumatano  timu hiyo ikikubali kutoa Pauni 60 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 8 milioni kama ada ya uhamisho ya kumsajili Eze.

Vilevile Spurs ilishafikia hadi  makubaliano binafsi na Eze mwenyewe na kilichokuwa kinasubiriwa ni asaini mkataba kisha ajiunge nao.

Hata hivyo, Palace iliomba Eze aendelee kubakia hadi atakapocheza mchezo wa Uefa Conference League dhidi ya Fredrikstad ya Norway, Alhamisi usiku.

Sasa wakati Spurs inaendelea kusubiri ikiamini kila kitu kipo sawa, hapo ndipo Arsenal ikaingilia kati Jumatano mchana na kuvuruga mpango wao.

Tottenham ilimgeukia Eze baada ya James Maddison kuthibitishwa atakosa sehemu kubwa ya msimu kutokana na jeraha kubwa la goti

Arsenal imelazimika kuingilia dili hili kutokana na jeraha la Kai Havertz aliliopata msimu huu.

 Arsenal imeonekana kushinda mbio hizo kwa mchezaji ambaye tangu utotoni amekuwa shabiki wa timu hiyo na mara zote inadaiwa alikuwa akitamani kucheza Emirates.

Hili linakuwa ni pigo lingine kwa Levy, ambaye tayari alishindwa kumnasa Morgan Gibbs-White baada ya kiungo huyo kusaini mkataba mpya na Nottingham Forest.

Iwapo usajili huu wa Eze kwenda Arsenal utakamilika, Spurs italazimika kusaka kiungo mshambuliaji mpya kwani James Maddison anatarajiwa kukosa sehemu kubwa ya msimu.

Awali, Arsenal ilipunguza nia yao kwa Eze baada ya kumsainisha mkataba mpya na kinda Ethan Nwaneri.

Ikiwa dili hili litakamilika, litafanya matumizi ya Arsenal katika dirisha hili la majira ya kiangazi kufikia takribani Pauni 250 milioni na ataungana na mastaa wengine walioingia hivi karibuni kama Kepa Arrizabalaga, Cristhian Mosquera, Martin Zubimendi, Christian Norgaard, Noni Madueke na Viktor Gyokeres.

Aliichezea dakika 84 kwenye sare ya 0-0 dhidi ya Chelsea Jumapili na alihudhuria mazoezi Jumatano kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa.

Eze pamoja na nahodha wa Palace, Marc Guehi ambaye pia anahusishwa na Liverpool, wote wanatarajiwa kucheza kwenye mechi ya kwanza ya mtoano ya kimataifa itakayopigwa  huko Selhurst Park.

Kocha wa Palace, Oliver Glasner, alisema:”Wengi mtashangaa kuona wakiendelea kuanza, licha ya tetesi zote. Wamejitolea kuwa hapa na watakuwa sehemu muhimu ya kikosi. Wamejitolea kwa ajili ya timu, na wakiondoka, wanataka kukumbukwa kama wachezaji waliojitoa kwa asilimia mia.”