Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Spurs jino kwa jino dili la Scott McTominay

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Wiki kadhaa zilizopita taarifa kutoka Italia zilidai staa huyo anatamani kurudi England kwa sababu amechoshwa na maisha ya Napoli ambako hayupo huru hata kutembea kutokana na kuwa staa wa timu na muda wote akionekana nje kundi la watu linamfuata kutaka kupiga naye picha na kupata saini yake.

ARSENAL inatazama uwezekano wa kumsajili kiungo wa Napoli na timu ya taifa ya Scotland, Scott McTominay, 28, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Wiki kadhaa zilizopita taarifa kutoka Italia zilidai staa huyo anatamani kurudi England kwa sababu amechoshwa na maisha ya Napoli ambako hayupo huru hata kutembea kutokana na kuwa staa wa timu na muda wote akionekana nje kundi la watu linamfuata kutaka kupiga naye picha na kupata saini yake.

Tottenham Hotspur na Everton ni miongoni mwa timu ambazo zinafikiria kumsajili, lakini hakuna iliyofikia mwafaka hadi sasa ingawa Arsenal inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumpata.

Mctominay ambaye amewahi kuwa MVP wa Napoli katika msimu wake wa kwanza alipojiunga nayo akitokea Manchester United mbali ya masuala ya umaarufu pia anataka kurudi England kwa sababu ya familia kwani hadi sasa bado ipo nchini humo. Mkataba wake Napoli unamalizika 2028.


Ousmane Diomande

CRYSTAL Palace inataka kuanza tena upya mazungumzo na wawakilishi wa beki kisiki wa  Sporting Lisbon, Ousmane Diomande ili kumsajili dirisha lijalo la majira ya baridi. Mabosi wa Palace wanamwangalia kama mbadala wa Marc Guehi, 25, ambaye anatarajiwa kuondoka katika dirisha lijalo au mwisho wa msimu. Diomande ambaye ni miongoni mwa mabeki tegemeo wa Lisbon na timu ya taifa ya Ivory Coast amewahi pia kuhitajika Chelsea.


Elliot Anderson

MANCHESTER United inatamani kumsajili kiungo wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya England, Elliot Anderson, 23, ili akawe mbadala wa Casemiro ambaye anahusishwa kuondoka mwisho wa msimu huu. Hata hivyo, mpango wa Man United unakumbana na upinzani kutoka Liverpool na Newcastle United ambazo pia zinahitaji huduma yake. Taarifa zinaeleza mabosi wa Forest wanahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni ili kumuuza.


Antoine Semenyo

LIVERPOOL, Tottenham Hotspur, Manchester United, Manchester City na Arsenal zote zinamenyana ili kumsajili winga wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, 25. Vigogo hivyo vinatamani saini ya Semenyo Januari kwa sababu taifa lake halijafuzu kucheza michuano ya Afcon. Licha ya utitiri wa timu zinazomhitaji inaelezwa Liverpool ndio ina nafasi kubwa zaidi kuipata huduma yake.


Emiliano Martinez

INTER Milan inataka kumsaiili kipa wa Aston Villa na timu ya taifa ya Argentina, Emiliano Martinez, 33, dirisha lijalo la kiangazi. Katika dirisha lililopita la kiangazi alikuwa karibu kujiunga na Man United, lakini dili lilifeli na badala yake ikamsajili kipa wa Royal Antwerp, Sanne Lammes. Inter ipo tayari kutoa Euro 40 milioni ili kumsajili Martinez ambaye mkataba wake unamalizika 2028.


Bukayo Saka

ARSENAL ipo karibu kukamilisha mchakato wa kumsainisha mkataba mpya wa muda mrefu staa wake wa kimataifa wa England, Bukayo Saka ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027. Katika mkataba Saka atakuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri zaidi kwenye Ligi Kuu England. Saka amekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Arsenal katika Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Matteo Guendouzi

SUNDERLAND bado inatamani kumsajili kiungo wa Lazio na timu ya taifa ya Ufaransa, Matteo Guendouzi, mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha lijalo. Inaelezwa staa huyo anaweza kuuzwa kwa takribani Pauni 26 milioni. Guendouzi kwa sasa yupo Lazio kwa mkopo kutoka Marseille lakini ana kipengele cha kununuliwa moja kwa moja.


Jean Philippe Mateta

CRYSTAL Palace imeanza mazungumzo kumsainisha mkataba mpya straika raia wa Ufaransa, Jean-Philippe Mateta ili kuendelea kusalia katika kikosi baada ya kuona timu nyingi zinahitaji saini yake. Mateta, 28, katika dirisha lililopita la majira ya baridi ya kiangazi alikuwa akitajwa kuwa katika rada za Manchester United lakini dili hilo liliota mbawa.