Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Man City acha tuone shoo

Muktasari:

  • Arsenal ambayo ndiyo wenyeji wa mchezo huo wa raundi ya tano ya ligi hiyo maarufu duniani kwenye Uwanja wa Emirates, unaotarajiwa kuanza saa 12:30 jioni, itawakosa nyota wake Gabriel Jesus ambao wanaendelea na programu za mazoezi mepesi kabla ya kurejea rasmi uwanjani.

LONDON, ENGLAND: ILE siku ndo leo. Baada ya miamba ya soka Arsenal na Manchester City kushinda mechi zao mbili za mwisho za Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya, mashabiki wa timu hizo wamekuwa wakitambiana kabla ya kukutana leo kumaliza ubishi, huku kila moja ikiwa na hofu ya majeruhi ilionao.

Arsenal ambayo ndiyo wenyeji wa mchezo huo wa raundi ya tano ya ligi hiyo maarufu duniani kwenye Uwanja wa Emirates, unaotarajiwa kuanza saa 12:30 jioni, itawakosa nyota wake Gabriel Jesus ambao wanaendelea na programu za mazoezi mepesi kabla ya kurejea rasmi uwanjani.

Kwa upande wa Man City, kuna mashaka kwa baadhi ya wachezaji, akiwamo mshambuliaji Rayan Cherki na ataendelea kuwa nje kwa muda kutokana na jeraha la paja, Omar Marmoush naye hatokuwepo, Huku kiungo Mateo Kovacic mwenye jeraha la kifundo cha mguu (Achilles) atakosekana sambamba na Kalvin Phillips ambaye ana jeraha kama hilo.

Hata hivyo, Majeruhi sio ishu sana na haizuii mechi hiyo kuchezwa na kinachosubiriwa na nani ataibuka mbabe kati ya Washika Mitutu wa London wanaokamata nafasi ya pili na pointi tisa, wakishinda tatu na kupoteza mmoja, nyuma kwa pointi tatu kwa Liverpool ambayo jana ilikipiga na Everton, na Man City iliyo nafasi ya nane ikishinda mbili kati ya nne na ina pointi sita, zote zikiwa zimeshacheza mechi nne.

Nyota wengine, Ben White, Bukayo Saka, na Martin Odegaard bado wana hatihati ya kucheza na katika na waandishi wa habari kabla ya mechi ya leo, Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alisema: “Kama kuna uwezekano tutajua baada ya mazoezi ya kesho (jana) kwa sababu bado hali sio nzuri na hawapo tayari kwa sasa.”

“Kila kitu kimekuwa kikibadilishwa kwa ajili yao, lakini bado kuna mambo kadhaa ya kufanyiwa kazi na kesho tutajua kama watakuwa sehemu ya kikosi au la.”

Pia sintofahamu kuhusu beki William Saliba ambaye alikuwa benchi wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Athletic Club Jumanne usiku.

Arteta alisema: “Tutaona. Ni wazi bado ana majeraha. Amejitahidi sana kuwa tayari ili kucheza mechi iliyopita. Anajituma kweli, kwa hiyo tutaamua ikiwa acheze kwa dakika ngapi katika mchezo huo.”

Hata hivyo, kulikuwa na habari njema baada ya Arteta kuthibitisha kwamba mshambuliaji Viktor Gyokeres na kiungo Mikel Merino watakuwa tayari kwa ajili ya mechi ya leo baada ya kupona majeraha madogo ya kichwa waliyoyapata katikati ya wiki kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Athletic Club.

Man City pia wamepata faraja baada ya beki John Stones kurejea kwenye kikosi.

Beki huyo ambaye alionekana akifanya mazoezi kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Alhamisi, hakujumuishwa katika kikosi kilichocheza mechi hiyo lakini sasa yupo fiti.

Mchezaji mmoja anayetarajiwa kurejea ni Rayan Ait-Nouri aliyepata maumivu ya kifundo cha mguu dhidi ya Tottenham.  Mbali ya mechi ya leo, Sunderland ambayo imeanza ligi vizuri itakuwa nyumbani kuikaribisha Aston Villa wakati Bournemouth ikiwa mwenyeji wa Newcastle, mechi zote zitaanza saa 10:00 jioni.