Arsenal Barcelona vitani saini ya Rashford
Muktasari:
- Inaelezwa kwamba mchezaji huyo aliyewahi kuzichezea Aston Villa na Barcelona kwa mkopo katika misimu miwili iliyopita ado haridhishwi na maisha ndani ya Manchester United hasa kutokana na alivyochukuliwa kipindi cha kocha Ruben Amorin.
MANCHESTER United haijaondoa uwezekano wa mshambuliaji wa kimataifa wa England, Marcus Rashford, kuondoka katika klabu hiyo, huku Arsenal na Barcelona zikiendelea kufuatilia kwa karibu hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.
Inaelezwa kwamba mchezaji huyo aliyewahi kuzichezea Aston Villa na Barcelona kwa mkopo katika misimu miwili iliyopita ado haridhishwi na maisha ndani ya Manchester United hasa kutokana na alivyochukuliwa kipindi cha kocha Ruben Amorin.
Hata hivyo, vigogo wa Old Trafford wanadaiwa kwamba katika siku za karibuni wamekuwa wakikutana mara kwa mara na mchezaji huyo kumtaka abaki kikosini ili awasaidie katika juhudi za kukirejeshea ubora wakati huu kkipambana kujiweka sawa kwa ajili ya michuano ya kimataifa ijayo.
Manchester United inatarajia kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya zaidi ya misimu mitano kupita.
Kwa upande wa barcelona, inadaiwa kwamba imeanz atena kumfukuzia Rashford dakika hizi za lalasalama kabla ya dirisha la usajili kufungwa kutokana na uwezo wake wa kucheza kama mshambuliaji wa kati na pembeni.
Mpaka sasa timu hiyo haijaziba pengo lililoachwa na straika, Robert Lewandowski aliyeondoka.
VUK PAVICEVIC
INTER Milan wameamua kutoendelea na mpango wa kumsajili kiungo wa OFK Grbalj na timu ya taifa ya Montenegro, Vuk Pavicevic, kwa ajili ya kikosi cha U23 licha ya mazungumzo ya awali kufikia hatua za juu. Kwa sasa nyota huyo aliyezaliwa 2008 yupo mbioni kujiunga na Atalanta, ambao kwa sasa wanaongoza mbio za kumsajili.
TONI FERNANDEZ
VENEZIA inadaiwa kufikia makubaliano ya awali ya kumsajili Toni Fernández kutoka Barcelona. Makubaliano yamefikiwa kwa ada ya uhamisho ya Euro 4 milioni, huku Barcelona ikipata asilimia 50 ya fedha za mauzo ya mchezaji huyo endapo atauzwa baadaye. Pia kuna kipengele cha kumnunua tena.
MOISE KEAN
COMO inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Fiorentina na timu ya taifa ya Italia, Moise Kean katika dili linaloweza kufikia takriban Pauni 35 milioni. Mazungumzo yanaendelea vizuri, huku Kean akionekana kuwa karibu zaidi kuhamia Como katika dirisha hili la usajili.
ERIK LIRA
AS Monaco inadaiwa kufikia makubaliano ya awali kwa njia ya mazungumzo kuhusu kumsajili kiungo wa Cruz Azul na Mexico, Erik Lira. Monaco inadaiwa kuwa tayari kulipa ada ya uhamisho ya Euro 8 milioni huku Cruz Azul ikiweka kipengele cha asilimia 20 ya mauzo ya mchezaji huyo siku za usoni.
Hatua ya mwisho iliyosalia ni AS Monaco kupata nafasi ya ziada kwenye kikosi chao, baada ya hapo mchakato wa uhamisho utaendelea hadi hatua ya kusaini mikataba.
NICK WOLTEMADE
NAPOLI inafikiria kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Newcastle United na timu ya taifa ya Ujerumani, Nick Woltemade, 24. Klabu hiyo ya Italia imeanza kutathmini uwezekano wa kumchukua Woltemade kwa mfumo wa mkopo katika dirisha hili la usajili.
DANIEL MUNOZ
NOTTINGHAM Forest imewasilisha ofa yenye thamani ya hadi pauni22 milioni kwa ajili ya kumsajili beki wa pembeni wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Colombia, Daniel Munoz, 30. Forest imechukua hatua hiyo katika jitihada za kuimarisha kikosi chake kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
IGOR JESUS
ATLETICO Madrid inafikiria kumsajili mmoja au wote kati ya washambuliaji wa Brazil, Igor Jesus, 25, wa Nottingham Forest na Gabriel Jesus, 29, wa Arsenal ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
ILIMAN NDIAYE
MANCHESTER City imemtaja kiungo mshambuliaji wa Everton, Iliman Ndiaye, 26, kuwa mmoja wa wachezaji wanaolengwa katika usajili, lakini klabu hiyo imemuweka kwenye thamani ya takribani pauni80 milioni. Ndiaye, raia wa Senegal, amekuwa akifuatiliwa na City kutokana na uwezo wake wa kucheza kiungo mshambuliaji.
Exequiel Palacios
IPSWICH Town imetangaza kumsajili kiungo wa kimataifa wa Argentina, Exequiel Palacios kutoka Bayer Leverkusen kwa ada ambayo haijawekwa wazi. Palacios, 27, amesaini mkataba wa kuichezea Ipswich Town hadi 2030 na atavaa jezi ya klabu hiyo kuanzia msimu huu.