Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arbeloa apewa mechi mbili Fulham

ARBELOA Pict

Muktasari:

  • Arbeloa anakabiliwa na wakati mgumu baada ya Fulham kushuka hadi mkiani mwa msimamo wa Premier League kufuatia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ipswich Town, Jumamosi, katika mchezo ambao walishindwa kulinda uongozi wao na kuruhusu bao la ushindi kufungwa dakika za mwisho.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Fulham, Alvaro Arbeloa, 43, anaripotiwa kuwa hatarini kutimuliwa, miezi mitatu tu baada ya kupewa mikoba ya kuinoa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Arbeloa anakabiliwa na wakati mgumu baada ya Fulham kushuka hadi mkiani mwa msimamo wa Premier League kufuatia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ipswich Town, Jumamosi, katika mchezo ambao walishindwa kulinda uongozi wao na kuruhusu bao la ushindi kufungwa dakika za mwisho.

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la The Standard, aliyekuwa beki wa zamani wa Liverpool, Arbeloa, amepewa michezo miwili pekee kuokoa ajira yake, kufuatia mwanzo mbaya wa msimu akiwa na kikosi hicho cha London Magharibi.

ARB 02

Viongozi wa Fulham wanadaiwa kuwa tayari kuchukua uamuzi wa kuachana naye iwapo hatapata matokeo mazuri katika mechi zijazo dhidi ya Hull City na Coventry City, timu zilizopanda daraja hivi karibuni.

Arbeloa aliteuliwa kuiongoza Fulham baada ya kocha Marco Silva kukataa kusaini mkataba mpya na kuhamia Benfica wakati wa majira ya joto.

Hata hivyo, tangu atue Craven Cottage, kocha huyo raia wa Hispania bado hajapata ushindi wake wa kwanza katika Premier League, hali inayozidi kuongeza presha juu ya mustakabali wake ndani ya klabu hiyo.

Fulham haijashinda katika michezo yake sita ya kwanza ya ligi msimu huu, huku ushindi wao pekee ukipatikana katika michuano ya Carabao Cup walipoifunga West Ham, inayowania kupanda daraja kutoka Championship.

ARB 03

Mbali na matokeo mabaya, Arbeloa pia amekuwa akikosolewa kutokana na maamuzi yake ya kufanya mabadiliko ya wachezaji wakati wa mechi. Timu yake imeruhusu mabao katika dakika 15 za mwisho za mchezo katika mechi nne kati ya sita ilizocheza kwenye ligi.

Kocha huyo pia aliwahi kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu kufuatia sare dhidi ya Manchester United mwezi uliopita.

Pamoja na presha hiyo, Arbeloa amesisitiza kuwa hana hofu ya kupoteza kazi yake, akieleza kuwa kipaumbele chake ni kuhakikisha Fulham inapata matokeo yanayohitajika.

Akizungumza baada ya kipigo dhidi ya Ipswich, amesema: “Sijawahi kuwa na wasiwasi kuhusu nafasi yangu. Sina hofu. Huwezi kuwa kocha ikiwa unaishi kwa hofu.

“Unapaswa kufanya kazi, kufanya maamuzi na kuwaonyesha wachezaji wako kuwa una imani nao.

ARB 01

“Kwa upande wangu, ninafurahishwa na mambo mengi ambayo wachezaji wangu wanafanya. Najua si rahisi kwao.

“Jambo muhimu si nafasi yangu, bali ni nafasi ya Fulham. Hilo ndilo la msingi zaidi. Ni kweli tumecheza mechi sita tu, lakini pia ni wazi tunahitaji pointi.”

Kwa sasa, Fulham iko pointi mbili nyuma ya eneo la usalama na inatarajiwa kukabiliana na Hull City Jumamosi, katika mchezo ambao unaweza kuwa na umuhimu mkubwa kwa hatima ya Arbeloa.

Iwapo taarifa hizo zitathibitishwa na uongozi wa klabu, michezo miwili ijayo inaweza kuwa kipimo muhimu kwa kocha huyo katika juhudi zake za kuokoa ajira yake na kuirejesha Fulham kwenye mstari wa ushindani.