Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi mbili zampa kiburi Barker

BARKER Pict

Muktasari:

  • Simba ambayo imekusanya pointi 21 katika mechi saba za Ligi Kuu Bara, ikifunga mabao 13, ilimaliza msimu uliopita ikiwa na mataji mawili ya Kombe la CRDB na Kombe la Muungano chini ya Barker lakini ikakosa ubingwa wa ligi kwa tofauti ya pointi mbili nyuma ya Yanga huku safari yake ya kimataifa ikiishia hatua ya makundi.

KOCHA wa Simba, Steve Barker, amesema kikosi chake kina uwezo wa kufanya makubwa zaidi msimu huu, akitaja ushindi dhidi ya Yanga na Azam kuwa ishara ya hatua inayopiga timu hiyo, lakini akisisitiza kuwa bado haijafika wakati wa kuridhika na matokeo ya mwanzo wa msimu.

Simba ambayo imekusanya pointi 21 katika mechi saba za Ligi Kuu Bara, ikifunga mabao 13, ilimaliza msimu uliopita ikiwa na mataji mawili ya Kombe la CRDB na Kombe la Muungano chini ya Barker lakini ikakosa ubingwa wa ligi kwa tofauti ya pointi mbili nyuma ya Yanga huku safari yake ya kimataifa ikiishia hatua ya makundi.

Safari hii, Wekundu hao wa Msimbazi wameanza kwa ushindi katika mechi zote saba, wakipata matokeo yanayowaweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa na kuongeza matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya Afrika huku kocha huyo akiweka rekodi ya kucheza mechi 33 bila kupoteza.

HISI 01

“Kupata matokeo mazuri dhidi ya wapinzani wako kama vile Yanga na Azam ni jambo zuri kwetu. Nimewaambia wachezaji wangu kwamba huu ni mwanzo na msimu huwa na mechi nyingi mbele, hivyo bado kuna kazi ngumu na kubwa ya kufanya,” amesema kocha huyo na kuongeza;

“Kwa sasa, hesabu zetu ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri dhidi ya Mashujaa ili kuendeleza mwenendo wetu katika mechi zilizopita, tunatambua kuwa ni moja ya timu ngumu, hivyo tunatakiwa kuwa kwenye kiwango chetu. Baada ya mchezo huo, ndipo tutaelekeza nguvu zetu kwenye mechi ya kimataifa. Ni muhimu kwetu kwenda hatua kwa hatua.”

HISI 03

Katika mechi saba za ligi, Simba imeifunga Kagera Sugar mabao 2-0, Pamba Jiji 2-1, Singida Black Stars 2-1, Coastal Union 1-0, Geita Gold 2-0, Azam FC 2-0 na Yanga 2-1. Matokeo hayo yanaifanya kuwa na wastani wa karibu mabao mawili kwa kila mchezo.

Baada ya kukabiliana na Mashujaa leo,  Simba itakuwa na kibarua kizito katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambako inatarajiwa kucheza ugenini mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya 15 de Agosto ya Equatorial Guinea.