Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AMORIM: Kazi ngumu Man United inamlipa Sh21 bilioni kwa mwaka

ATM Pict

Muktasari:

  • Ndiye aliyebebeshwa mzigo wa kuinoa Manchester United kwa sasa. Kwa ukubwa wa Man United, ikishinda ni shida, ikifungwa ni shida hata ikitoka sare ni shida, hivyo jina hilo litabamba tu kwenye vyombo vya habari.

LONDON, ENGLAND: Ruben Filipe Marques Amorim. Si jina geni kwenye masikio ya mashabiki wa mchezo wa soka duniani.

Ndiye aliyebebeshwa mzigo wa kuinoa Manchester United kwa sasa. Kwa ukubwa wa Man United, ikishinda ni shida, ikifungwa ni shida hata ikitoka sare ni shida, hivyo jina hilo litabamba tu kwenye vyombo vya habari.

Akizaliwa, Januari 27, 1985, huko Ureno, Amorim anakabiliwa na kibarua kigumu sana cha kuweka mambo sawa kwenye kikosi cha Man United, ambayo kwa sasa inapambana kutoangukia kwenye janga la kuangukia kwenye shimo la kushuka daraja.

Lakini, wakati ukiwaza presha inayomkabili kocha huyo kwenye kurudisha makali ya Man United, mwenyewe anaweza kujipoza vyema kutokana na kile kinachoingia kwenye akaunti yake ya benki, mkwanja wa maana.

AT 02

Amorim amebakiza siku chache kufikisha umri wa miaka 40, lakini anaripotiwa kuwa na pato la Pauni 13 milioni. Ndiyo hivyo, Pauni 13 milioni kwa pesa ya Kitanzania ni kama Sh42.4 bilioni kwa pesa ya Kitanzania.

AT 04

AMEPIGAJE HUO MKWANJA

Kazi kubwa ya Amorim ni soka. Alianza kupiga pesa tangu akiwa mchezaji. Wakati anacheza, Amorim alikuwa kiungo. Sehemu kubwa ya maisha yake ya soka alicheza huko Ureno, kwenye vikosi vya Belenenses na Benfica.

Hata hivyo, Amorim hakucheza kwa muda mrefu, alistaafu mapema na kuingia kwenye ukocha, ambao ndiyo kazi yake kwa sasa. Machi, 2020, Amorim alichaguliwa kuwa kocha wa Sporting CP na hapo, akawa kocha namba tatu ghali zaidi. Sporting ililipa Pauni 8.4 milioni kupata huduma yake.

Mafanikio ya ndani ya uwanja, yalimfanya Amorim ashinde tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka kwenye Ligi Kuu Ureno, kitu ambacho kiliwafanya Man United kwenda kunasa saini yake mwishoni mwa mwaka 2024.

Man United ililipa Pauni 9 milioni kupata saini yake na alipotua Old Trafford, imekwenda kumpa dili la kumlipa mshahara wa Pauni 6.5 milioni kwa mwaka. Kwa maana hiyo, Amorim analipwa Sh21 bilioni kwa mwaka.

Mshahara huo unamfanya Amorim kuwa kwenye 15 bora ya makocha wanaolipwa vizuri duniani, akiwa kwenye kundi moja na makocha mashuhuri kama Pep Guardiola, lakini akiwazidi Xabi Alonso, Simone Inzaghi na Thomas Tuchel kwa mshahara wake anaolipwa kwenye kuinoa timu ya taifa ya England.

Amorim alipokuwa Sporting CP alikuwa akilipwa Pauni 3 milioni kwa mwaka, lakini alipotua Man United, alizidisha mshahara huo zaidi ya mara mbili na kuvuna mkwanja wa maana kabisa.

AT 01

MREMBO MARIA ANAMPA MZUKA

Amorim alifunga pingu za maisha na mrembo Maria Joao Diogo tangu mwaka 2013 baada ya kufanya sherehe kubwa iliyofanyika Coimbra, ambayo ilihudhuriwa na majina makubwa ya wanasoka wa Ureno. Wawili hao wameamua kuishi maisha yao ya ndoa kuwa binafsi. Mrembo Maria, naye anajishughulisha na mambo mengi, akiwa mbunifu wa mitindo ya mavazi na mfanyabiashara. Amorim na Maria wamefanikiwa kupata watoto wawili. Familia ya Amorim imejaa watu wa mpira. Mkewe, mrembo Maria yao ni ya wanasoka pia, akiwamo beki Luis Filipe na mkurugenzi wa soka wa zamani wa klabu ya Paris Saint-Germain, Antero Henrique, ndiye aliyefanya mambo kwenye usajili wa kumnasa Neymar kutoka Barcelona kwenda Parc des Princes.

Mke wa Amorim ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya mitindo ya Dois Tons, aliyoanzisha mwaka 2019 sambamba na mrembo Raquel Viana, mke wa mkurugenzi wa soka wa zamani wa Sporting, Hugo Viana.

AT 03

MAKAZI YAKE NA USAFIRI

Baada ya kutua Manchester, Amorim alifikia kwenye hoteli ya kitalii ya The Lowry Hotel, iliyopo Salford, Greater Manchester, Amorim alifuata nyayo za Mreno mwenzake, Jose Mourinho wakati alipotua Man United, ambapo aliishi kwenye hoteli hiyo kwa siku 895 na kugharimu Pauni 500,000.

Amorim naye aliishi kwenye hoteli hiyo, akilala kwenye chumba chenye hadhi ya urais, ambapo kwa usiku mmoja ni Pauni 4,000 sawa na Sh13,038,240 za Kitanzania. Ndio, usiku mmoja, Sh13milioni. Lakini, hivi karibuni, iliripotiwa kupata nyumba kwenye mtaa wa kibosi, ambako atakuwa huru kuishi na familia yake.

Kwenye mambo ya usafiri, Amorim ni mpenzi wa ndinga za kifahari aina ya Porsche. Alikuwa akiendeesha gari ya aina hiyo huko Ureno na hata alipohamia England, alionekana akiwasili mazoezini Man United huko Carrington, akiwa na Porsche Taycan Turbo Estate, yenye thamani ya Pauni 180,000.