Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim: Hata aje Papa sibadili mfumo

Muktasari:

  • Amorim hajaonyesha majuto licha ya kuanza vibaya zaidi msimu huu ikiwa ni kwa mara ya kwanza baada yamiaka 33.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim amesisitiza hata aje Papa hawezi kumshawishi kubadilisha mtindo wake wa kucheza.

Amorim hajaonyesha majuto licha ya kuanza vibaya zaidi msimu huu ikiwa ni kwa mara ya kwanza baada yamiaka 33.

Tajiri wa Man United, Sir Jim Ratcliffe alitua kwa helikopta Carrington Alhamisi kwa ajili ya mazungumzo na kocha huyo, Afisa Mtendaji Mkuu Omar Berrada na Mkurugenzi wa michezo Jason Wilcox na inaelezwa hata baada ya mazungumzo hayo Amorim alikataa  kubadilisha mbinu zake.

"Hapana, hapana, hapana. Hakuna mtu. Hata Papa hawezi kunibadilisha. Hii ni kazi yangu. Huu ni wajibu wangu. Haya ni maisha yangu. Kwa hiyo sitabadilisha," alisema.

"Kama mimi ni mchezaji na nina kocha ambaye, akiwa chini ya presha kubwa, akaambiwa 'unahitaji kubadilisha mfumo' na mimi nikakubali, katika wakati huu wachezaji wataniona kwa mtazamo tofauti. Naamaini kutakuwa na mabadiliko taratibu, lakini tunahitaji kuchukua hatua sahihi na kuvumilia. Ninafanya mambo kwa njia yangu."

Kuhusu mazungumzo na Ratcliffe, Amorim alitania: "Alinipatia mkataba mpya! Hapana, ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida ya kuonyesha ananiunga mkono, kuniambia huu ni mradi wa muda mrefu, jambo ambalo amekuwa akilisema mara nyingi. Tulizungumza mambo ya kawaida na Omar na Jason."

"Kwa sasa naelewa, ni  kawaida watu kutoa macho kwenye hili. Hii ni klabu ya mpira yenye presha kubwa zaidi kuliko nyingine yoyote duniani na siku zote tunataka kushinda."

Wakati presha ikiendelea kuwa kubwa kwa kocha huyo kutokana na matokeo, Mgombea urais wa Benfica, Joao Noronha Lopes, alikuwa England kushuhudia Manchester derby akiwa na wapambe wake na katika kampeni zake aliweka wazi anaweza kumrudisha Amorim tena Ureno ingawa jambo hilo huenda lisifanikiwe kwani Rui Costa, rais wa sasa, alichukua hatua kumfukuza Bruno Lage na kumwajiri Jose Mourinho wiki hii.

Amorim pia alipoulizwa kama alitafutwa na viongozi wa timu hiyo alisema: "Hapana jamani, hakuna mawasiliano na mnaona tayari Mourinho yupo pale," alisema kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon.