Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim atoa onyo kali Man United

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Mabao kutoka kwa Bruno Fernandes na Casemiro yaliisaidia Man United kushinda 2-1 katika mchezo huo ambao ulikuwa wa pili kushinda tangu kuanza kwa msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim wamewapa onyo wachezaji wake licha ya kuibuka na ushindi dhidi ya Chelsea wikindi iliyopita.

Mabao kutoka kwa Bruno Fernandes na Casemiro yaliisaidia Man United kushinda 2-1 katika mchezo huo ambao ulikuwa wa pili kushinda tangu kuanza kwa msimu huu.

Mashetani wekundu hao walitumia vizuri fursa baada ya kipa Robert Sanchez kuonyeshwa kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza.

Casemiro kwa upande wa Man United pia aliondolewa kwa kadi nyekundu hali iliyosababisha Chelsea kurudi mchezoni hata kupata bao kupitia kwa Trevoh Chalobah.

Amorim alifurahia kupata ushindi lakini aliwaonya wachezaji wa timu hiyo kwamba ushindi huo hautokuwa na maana ikiwa hawataendelea kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo.

"Sasa ni wakati wa kuendelea kupata matokeo mazuri. Tulistahili ushindi, lakini huu ni ushindi mmoja tu na tunahitaji kufikiria kuhusu mechi ijayo. Ushindi huu ulikuwa ni muhimu sana kwa sababu ya mazingira yanayonizunguka mimi kama kocha na timu kwa ujumla. Kwangu naiona kama ni mechi ya kawaida tu ambayo ilishuhudiwa Manchester United ikishinda na kuvuna pointi tatu."

"Hatuwezi kusahau kuwa tunaweza kupoteza pia kama tulivyoshinda, tulipoteza dhidi ya Grimsby na tunaweza kushinda dhidi ya timu yoyote. Tunahitaji kuingia na akili hiyo kwa wiki ijayo. Najua ni jambo zuri kushinda, lakini sasa itabidi tusahau, tujue kwamba tunaweza kupoteza, tukifanya hivyo itatuletea hali ya kupambana zaidi, badala ya kubweteka."

Ushindi huo uliiwezesha Man United kupanda hadi nafasi ya 10 kwa pointi saba ilizopata kwa kutoa sare moja na kushinda mechi mbili kati ya tano za Ligi Kuu England msimu huu.

Chelsea imeshuka hadi nafasi ya sita ikiwa na pointi nane.