Amad Diallo: Tunacheza kitimu zaidi
Muktasari:
- Nyota huyo wa klabu ya Manchester United, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo iliyowavusha Ivory hadi robo fainali na sasa wanakabiliwa na Misri wikiendi hii.
MARRAKECH, MOROCCO: WATETEZI Ivory Coast imejihakikisha kwa ustadi nafasi katika robo fainali za michuno ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuichapa Burkina Faso 3-0 katika Grand Stade de Marrakech, huku nyota wa timu hiyo Amad Diallo, aliyeifungia timu bao zuri na kutoa pasi ya moja ya mabao hayo akisisitiza timu yako inacheza kwa umoja.
Nyota huyo wa klabu ya Manchester United, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo iliyowavusha Ivory hadi robo fainali na sasa wanakabiliwa na Misri wikiendi hii.
Katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi, winga huyo wa Man United alisisitiza nguvu ya pamoja ya mabingwa wa sasa:
"Kwanza, tunajaribu kupigana, kila mtu anajitahidi kuchangia kwa timu. Kisha tunakuwa na urafiki na mshikamano uwanjani. Tuko karibu sana, jambo ambalo linafanya mambo kuwa rahisi zaidi uwanjani," amesema, akisisitiza umoja unaowasukuma Tembo.
Aliongeza kuhusu ukarimu na usaidizi wa wachezaji wenzake: "Sisi hatutegemei mtu mmoja tu, kila mtu anapita pasi kwa mwenzake, hakuna anayetamani kung'ara peke yake. Ikiwa nina nafasi ya kumpa mwenzangu pasi, nampa. Ikiwa yeye ana nafasi ya kunipatia pasi, hunipatia. Hivyo ndilo linavyounda timu bora. Lazima tuchukue hatua pamoja kushinda mashindano haya. Haisi kazi ya nyota mmoja tu, bali ni kazi ya timu nzima uwanjani."
Nyota huyo pia alipongeza mchango wa kila mmoja katika kikosi: "Kuna nyota, kuna wachezaji wazuri sana. Pia kuna Bazoumana, ambaye alifunga amesema. Hivyo kila mtu anajaribu kuchangia. Hadi sasa, inafanya kazi kikamilifu."