Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alejandro Garnacho aziingiza vitani Tottenham, Chelsea

TETESI Pict

Muktasari:

  • Garnacho ana mkataba na Man United hadi Juni 2028 na kocha Ruben Amorim amempa ruhusa ya kuondoka kwa sababu haendani na mifumo yake.

TOTTENHAM Hotspur inajipanga kuingia katika kinyang’anyiro kuwania saini ya winga wa Manchester United na Argentina, Alejandro Garnacho, 21, ambaye pia anawindwa na Chelsea.

Garnacho ana mkataba na Man United hadi Juni 2028 na kocha Ruben Amorim amempa ruhusa ya kuondoka kwa sababu haendani na mifumo yake.

Hivi karibuni Chelsea iliripotiwa kufanya makubaliano binafsi na kinachosubiriwa ni kufikia mwafaka na Man United juu ya ada ya uhamisho.

Hata hivyo Spurs inataka kuingilia kati kuhakikisha inamdaka.
Licha ya kutamani kumpata, taarifa zinadai Garnacho ameshawaambia wawakilishi wake kuwa timu pekee anayotaka kujiunga nayo katika dirisha hili ni Chelsea.

Man United inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni kama ada ya uhamisho kwa timu itakayohitaji huduma yake.


Jorgen Strand Larsen
WOLVES inapambana kumbakiza mshambuliaji wake wa kimataifa wa Norway, Jorgen Strand Larsen, 25, anayehitajika na Newcastle United ambayo ipo tayari kulipa Pauni 60 milioni ili kumpata. Strand Larsen ana mkataba na Wolves hadi 2029, alijiunga na timu hiyo mwaka jana akitokea Celta Vigo.  Newcastle inamuona kuwa mbadala wa Alexander Isak anayelazimisha kuondoka dirisha hili.


Nathan Ake
EVERTON inavutiwa na beki kisiki wa Manchester City na Uholanzi, Nathan Ake, 30. Ake aliyejiunga na Man City 2020 akitokea Bournemouth kwa Pauni 41 milioni, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027. Everton inahitaji kuboresha safu ya ulinzi baada ya kuruhusu mabao 62 msimu uliopita. Hakuna taarifa kamili hadi sasa ikiwa Ake mwenyewe atakubali ofa hiyo.  


Jadon Sancho
LICHA ya taarifa za awali kudai winga wa Manchester United na England, Jadon Sancho, 25, amekataa ofa ya AS Roma, timu hiyo haijakata tamaa kumsajili. Kwa sasa mazungumzo yanaaendelea baina ya wakala wa Sancho na Roma lakini tatizo linaonekana kuwa kwa wakala ambaye anahitaji kamisheni ya Euro 10 milioni katika dili hilo. Mkataba wa Sancho unamalizika mwakani.


Antony

REAL Betis inapambana kuhakikisha inamsajili winga wa Manchester United na Brazil, Antony, 25, katika dirisha hili baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha msimu uliopita alipokuwa akiitumikia kwa mkopo. Hadi sasa hakuna uamuzi wowote uliofikiwa ikielezwa Man United inataka kumuuza jumla, wakati Betis ikimtaka kwa mkopo. Mkataba wa United na mchezaji huyo unaisha 2027.


Fabio Silva

BORUSSIA Dortmund inatarajia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno, Fabio Silva, 23, kutoka Wolves kabla ya wiki hii kumalizika. Silva alijiunga na Wolves 2020 akitoka FC Porto kwa ada iliyovunja rekodi ya usajili ya timu hiyo Pauni 35 milioni. Licha ya kusajiliwa kwa pesa nyingi ameshindwa kung’ara na imesababisha apelekwe kwa mikopo mara kadhaa kwenye timu kama PSV na Anderlecht.


Tyler Dibling
CRYSTAL Palace inataka kuipiku Everton kwenye dili la  kumsajili winga chipukizi wa England Tyler Dibling, 19, kutoka Southampton katika dirisha hili.Palace inataka kutoa karibu Pauni 35 milioni ili kufanikisha mchakato wa kumpata nyota huyo. Awali Everton ilidaiwa kuweka mezani Pauni 30 milioni, hivyo sasa itatakiwa kutoa zaidi ya kile kilichotolewa na Palace.


Nico Paz

TOTTENHAM Hotspur imemuongeza katika orodha kiungo wa Real Madrid anayecheza kwa mkopo Como ya Italia, Nico Paz pamoja na wa AS Monaco, Maghnes Akliouche katika dirisha hili kwa ajili ya kuziba pengo la James Maddison aliyekumbwa na majeraha ambayo yatamuweka nje kwa muda mrefu. Mpango uliopo sasa ni kuwasajili wote lakini ikishindikana atasajiliwa hata mmoja kati yao.