Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alan Shearer alimpua Bruno Fernandes

BRUNO Pict

Muktasari:

  • Foden alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 23 baada ya kumrushia mguu Fernandes, na kuiacha Manchester City ikicheza pungufu kwa sehemu kubwa ya mchezo wa Jumapili ambao mwisho City ilishinda bao 1-0.

LONDON, ENGLAND: GWIJI wa soka nchini England, Alan Shearer, amemshambulia nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, akimweleza kuwa amefanya kitendo cha “kusikitisha” katika tukio lililosababisha Phil Foden kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa Manchester Derby wikiendi iliyopita.

Foden alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 23 baada ya kumrushia mguu Fernandes, na kuiacha Manchester City ikicheza pungufu kwa sehemu kubwa ya mchezo wa Jumapili ambao mwisho City ilishinda bao 1-0.

Hata hivyo, Shearer anaamini Fernandes alichangia kwa kiasi kikubwa tukio hilo, baada ya kuonekana kumpiga Foden akiwa amelala chini, kabla ya kiungo huyo wa Manchester United kuanguka na kujizungusha uwanjani akionyesha maumivu.

“Namna Bruno Fernandes alivyoanguka ilikuwa ya kusikitisha,” Shearer akizungumza kwenye kipindi cha The Rest Is Football amesema.

“Alisaidia kumfanya Foden atolewe. Ndiyo, Foden alijaribu kumpiga, lakini Bruno pia alimpiga Phil Foden. Kama Foden angefanya alichofanya Bruno, wote wawili wangepata kadi nyekundu.”

BRUN 01

Shearer ambaye ni mchezaji wa zamani wa Newacastle amesisitiza kuwa mwamuzi Michael Oliver alipaswa kutoa adhabu sawa kwa wachezaji hao wawili.

“Kwa hiyo kwangu mimi, wote wawili walipaswa kupewa nyekundu au hakuna aliyepaswa kubaki. Kama Foden ni nyekundu, basi Bruno naye ni nyekundu,” amesema.

Mchambuzi mwingine wa soka, Gabby Agbonlahor, alikwenda mbali zaidi kwa kumtuhumu Fernandes kuwa ni mchezaji anayependa kudanganya waamuzi.

“Bruno Fernandes ni mdanganyifu. Ni mchezaji bora, lakini ni mdanganyifu,” amesema Agbonlahor kupitia talkSPORT.

BRUN 02

Kwa mujibu wa Agbonlahor, Fernandes alimpiga Foden mara mbili akiwa chini, lakini akaanguka na kujifanya ameumia baada ya Foden kujibu kwa kitendo kidogo.

Amesema mwamuzi angepaswa kuwaonya wote wawili na kuwapa kadi za njano badala ya kumtoa Foden kwa kadi nyekundu.


MWISHO WA ‘KARMA’

Agbonlahor pia alihusisha tukio hilo na bao la ushindi la Erling Haaland, ambalo liliipa Manchester City ushindi licha ya kuwepo kwa utata wa kuotea.

Enzo Fernandez alionekana kuingilia mchezo akiwa katika nafasi ya kuotea, lakini VAR ikaamua kuwa Haaland hakuwa ameotea.

BRUN 03

Baadaye, chombo rasmi cha waamuzi, Pro Ref, kilikiri kuwa kulikuwa na makosa katika uamuzi huo na kuwasiliana na Manchester United kuomba radhi.

Kwa mujibu wa maelezo yao, VAR ilipaswa kumshauri mwamuzi kwenda kwenye skrini ya uwanjani kupitia on-field review ili kutathmini upya ushawishi wa Fernandez katika tukio hilo.