Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al-Hilal yamnasa Summerville kwa Sh200 Bilioni

AL HILAL Pict

Muktasari:

  • Makubaliano hayo yanajumuisha malipo ya awali ya Pauni55 milioni, huku kiasi kingine cha Pauni5 milioni kikitegemea kufikiwa kwa vigezo mbalimbali vya kimkataba.

RIYADH,SAUDI ARABIA: KLABU ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imefikia makubaliano na West Ham United ya kumsajili winga wa kimataifa wa Uholanzi, Crysencio Summerville, kwa ada ya jumla ya Pauni 60 milioni (sawa na Sh200 bilioni).

Makubaliano hayo yanajumuisha malipo ya awali ya Pauni55 milioni, huku kiasi kingine cha Pauni5 milioni kikitegemea kufikiwa kwa vigezo mbalimbali vya kimkataba.

Summerville, mwenye umri wa miaka 24, sasa amepewa ruhusa ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake kwenda klabu hiyo ya jijini Riyadh.

Awali, West Ham ilikuwa imekataa ofa ya takribani Pauni40 milioni kwa nyota huyo, ambaye pia alihusishwa na kuwindwa na Aston Villa, lakini dau kubwa la Al-Hilal limeifanya klabu hiyo kubadili msimamo.

AL 01

West Ham yaendelea kuuza mastaa

Mauzo ya Summerville ni faida kubwa kwa West Ham, ambayo ilishuka daraja mwishoni mwa msimu uliopita.

Mwezi uliopita, klabu hiyo pia ilimuuza kiungo Mateus Fernandes kwenda Tottenham Hotspur kwa ada ya Pauni 85milioni.

Hata hivyo, West Ham imefanikiwa kumbakisha nahodha na mshambuliaji wake tegemeo Jarrod Bowen, ambaye amesaini mkataba mpya licha ya timu hiyo kushiriki Championship msimu wa 2026-27.

Baada ya kushuka daraja mwezi Mei, West Ham imekuwa ikifanya mabadiliko makubwa ya kifedha kwa kupunguza matumizi ya mishahara na kuongeza mapato kupitia mauzo ya wachezaji.

Pamoja na mabadiliko hayo, uongozi wa klabu umeamua kuendelea kumuamini kocha Nuno Espirito Santo, ambaye amepewa jukumu la kuiongoza timu hiyo katika harakati za kurejea Ligi Kuu msimu ujao.