Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tzolis anavyoingia kwenye mfumo wa Arteta

TZOLIS Pict

Muktasari:

  • Arsenal imekuwa ikitafuta mshambuliaji wa pembeni baada ya kuondoka kwa Leandro Trossard aliyejiunga na BeÅŸiktaÅŸ ya Uturuki kwa ada inayokadiriwa kuwa pauni milioni 15.3, na sasa inaonekana imepata mrithi wake.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 20, Arsenal imeanza harakati za kuimarisha kikosi chake ili kutetea taji hilo msimu ujao, huku jina la Christos Tzolis likiwa miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na kocha Mikel Arteta.

Arsenal imekuwa ikitafuta mshambuliaji wa pembeni baada ya kuondoka kwa Leandro Trossard aliyejiunga na BeÅŸiktaÅŸ ya Uturuki kwa ada inayokadiriwa kuwa pauni milioni 15.3, na sasa inaonekana imepata mrithi wake.

Taarifa kutoka England zinaeleza kuwa Arsenal imefikia makubaliano ya kumsajili Tzolis kutoka Club Brugge kwa ada ya pauni milioni 34, ambayo itakuwa rekodi mpya ya uhamisho katika historia ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ugiriki, amekuwa katika kiwango bora tangu alipojiunga na Club Brugge akitokea Norwich City mwaka 2024, akijijenga kama mmoja wa washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza mabao.

Katika misimu miwili akiwa na klabu hiyo ya Ubelgiji, Tzolis amefunga jumla ya mabao 33, lakini msimu wa 2025-2026 ndiyo uliomfanya kuvutia macho ya Arsenal.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliiongoza Club Brugge kutwaa ubingwa wa ligi baada ya kufunga mabao 17 na kutoa pasi 23 za mabao katika mechi 36.

Kwa jumla, alihusika moja kwa moja kwenye mabao 40, idadi ambayo ilikuwa juu kwa tofauti kubwa ukilinganisha na mchezaji mwingine yeyote katika ligi hiyo.

Moja ya mambo yaliyomvutia Arteta kwa Tzolis ni uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali katika safu ya ushambuliaji.

TZO 01

Mchezaji huyo anayependelea kutumia mguu wa kulia mara nyingi ameonekana akicheza upande wa kushoto wa ushambuliaji, lakini pia anaweza kutumika kama mshambuliaji wa kati, kiungo mshambuliaji au hata upande wa kulia.

Uwezo huo wa kubadilika ni aina ya sifa ambayo Arteta ameonyesha kuipenda kwa wachezaji wake.

Katika kikosi cha Arsenal, wachezaji wengi wamekuwa wakitumika katika nafasi tofauti kulingana na mahitaji ya mchezo, na Tzolis anaonekana kuendana na falsafa hiyo.

Tofauti na wachezaji wanaotegemea eneo moja pekee, Tzolis ana uwezo wa kubeba mpira, kuwafanyia presha mabeki na kutengeneza nafasi kwa wenzake.

Eneo lingine linaloweza kumfanya Tzolis kuwa muhimu Arsenal ni uwezo wake katika mipira iliyokufa.

Arsenal imekuwa moja ya timu bora zaidi duniani katika kutumia mipira ya kona na mipira ya adhabu.

Msimu wa 2025-2026, Arsenal iliweka rekodi ya kufunga mabao 19 kupitia mipira ya kona katika Ligi Kuu England. Tzolis naye ana uwezo mkubwa katika eneo hilo.

Kati ya nafasi 135 alizotengeneza akiwa Club Brugge msimu uliopita, nafasi 52 zilitokana na mipira iliyokufa, sawa na asilimia 38.5.

Uwezo huo unaweza kumsaidia kupata nafasi kwenye kikosi cha Arteta, hasa kutokana na changamoto za majeraha zinazowakabili baadhi ya wachezaji muhimu kama Bukayo Saka na Declan Rice.

TZO 01 (1)

Msimu uliopita ulikuwa wa kipekee kwa Tzolis kutokana na takwimu zake za kuvutia.

Katika wachezaji 13 waliomaliza msimu wa Ligi Kuu ya Ubelgiji wakiwa wamefunga mabao 10 au zaidi, Tzolis alikuwa kinara katika maeneo kadhaa muhimu.

Aliongoza kwa kutengeneza nafasi za kufunga akiwa na nafasi 135, alikamilisha chenga 40 na alifanya mipango ya kusogea na mpira mbele mara 359.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Tzolis si mfungaji pekee, bali ni mchezaji anayependa kushiriki katika ujenzi wa mashambulizi.

Hata hivyo, changamoto kubwa kwake itakuwa kuhamia kwenye mazingira magumu ya Ligi Kuu England.

Premier League inachukuliwa kuwa moja ya ligi zenye ushindani mkubwa zaidi duniani, tofauti na Ligi ya Ubelgiji ambayo kiwango chake ni cha chini ukilinganisha na England.

TZO 03

Hivyo, Tzolis atalazimika kuthibitisha haraka kwamba anaweza kufanya mambo yale yale aliyofanya Club Brugge.

Hata hivyo, Tzolis ameonyesha kuwa uwezo wake hauishii kwenye ligi ya ndani baada ya kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Akilinganishwa na Trossard katika mashindano hayo msimu uliopita, Tzolis alionyesha kuwa anaweza kuwa mbadala mzuri.

Ingawa Trossard alikuwa na mchango mkubwa zaidi wa mabao akiwa na mabao matano yaliyohusisha kufunga na kutoa pasi, Tzolis alionyesha ubora katika vipengele vingine vya mchezo.

Alikamilisha mipango 59 ya kupeleka mpira kuelekea eneo la ushambuliaji, zaidi ya Trossard aliyekuwa na 44. Pia alitoa pasi 26 zilizoingia eneo la mwisho la mashambulizi dhidi ya 16 za Trossard.

Tzolis pia alitengeneza nafasi 13 za kufunga, karibu mara mbili ya Trossard aliyekuwa na saba.

Ingawa Arsenal ina matumaini makubwa kwake, Tzolis atakuwa na kazi ya kuthibitisha uwezo wake baada ya Trossard kuacha pengo kubwa.

Trossard alipata umaarufu mkubwa Emirates kutokana na uwezo wake wa kuibuka katika mechi muhimu, ikiwemo kufunga bao lililosaidia Arsenal kutwaa ubingwa dhidi ya West Ham United.

Mashabiki wa Arsenal hawatatarajia Tzolis kufikia kiwango hicho mara moja, lakini umri wake mdogo na uwezo wake wa kukua chini ya Arteta vinaweza kuwa faida kubwa.

Usajili wa Tzolis huenda usiwe ule wenye jina kubwa ambao baadhi ya mashabiki walikuwa wanauhitaji, lakini unaweza kuwa usajili wa kimkakati wenye faida kubwa kwa Arsenal.

Kwa uwezo wa kufunga, kutengeneza nafasi, kutumia mipira ya adhabu na kucheza nafasi nyingi, Tzolis anaweza kuwa sehemu muhimu ya mipango ya Arsenal katika kutawala England na kufanya vizuri zaidi Ulaya.