Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bowen aamua kubaki West Ham

BOWEN Pict

Muktasari:

  • Bowen, aliyejiunga na West Ham akitokea Hull City mwaka 2020, amecheza jumla ya mechi 280 akiwa na The Hammers na kufunga mabao 85.

LONDON, ENGLAND: NAHODHA wa West Ham United, Jarrod Bowen, ataendelea kubaki katika klabu hiyo wakati timu hiyo ikijiandaa kucheza Ligi Daraja la Kwanza England (Championship) msimu ujao.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 29, alikuwa sehemu ya kikosi cha West Ham kilichoshuka daraja kutoka Ligi Kuu England baada ya kupoteza nafasi ya kubaki katika siku ya mwisho ya msimu, hali iliyozua mashaka kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo.

Bowen, aliyejiunga na West Ham akitokea Hull City mwaka 2020, amecheza jumla ya mechi 280 akiwa na The Hammers na kufunga mabao 85.

BOWE 01

Amepewa jukumu la unahodha tangu mwaka 2024 baada ya kuondoka kwa Kurt Zouma.

Mshambuliaji huyo pia ana mechi 22 akiwa na timu ya taifa ya England, ingawa hakuchaguliwa kwenye kikosi cha kocha Thomas Tuchel kilichokwenda kwenye Kombe la Dunia msimu huu.

Uamuzi wa Bowen kubaki umeleta faraja kubwa kwa West Ham ambao tayari wameanza maandalizi ya msimu mpya, wakiwa na lengo la kurejea Ligi Kuu England baada ya mara ya mwisho kucheza Championship msimu wa 2011-2012.

BOWE 02

Bowen ni mmoja wa wachezaji muhimu zaidi kwenye safu ya ushambuliaji ya West Ham. Msimu uliopita alianza kila mchezo wa Ligi Kuu England na alifunga mabao tisa.

Mchezaji huyo pia anakumbukwa kwa bao lake la ushindi alilofunga dakika ya mwisho dhidi ya Fiorentina katika fainali ya UEFA Europa Conference League mwaka 2023 mjini Prague, bao lililoipa West Ham taji lao la kwanza kubwa ndani ya miaka 43.

BOWE 03

Kabla ya kuthibitisha kubaki kwake, Bowen alikuwa akihusishwa na uhamisho wa majira ya kiangazi kwenda kwenye klabu nyingine ya Ligi Kuu England.

Hata hivyo, sasa ameonyesha dhamira ya kuendelea kuichezea West Ham msimu wa 2026-2027, ingawa bado hajatia saini mkataba mpya wa kuongeza muda wa huduma yake.

Mkataba wake wa sasa na klabu hiyo bado unaendelea hadi mwaka 2030.