Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aje Sesko, Gyokeres Arsenal

USAJILI Pict

Muktasari:

  • Na kwenye msako huo, Arsenal imeweka ubaoni majina mawili ya mastraika wa viwango vya dunia, mkali wa RB Lepizig, Benjamin Sesko na wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL inapambana kusaka kitu kinachokosekana kwenye kikosi chake, inasaka straika wa mabao ili kupiga hatua ya juu zaidi misimu mitatu iliyopita ambapo iliishia kumaliza kwenye nafasi ya pili mara tatu mfululizo.

Na kwenye msako huo, Arsenal imeweka ubaoni majina mawili ya mastraika wa viwango vya dunia, mkali wa RB Lepizig, Benjamin Sesko na wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres.

Kocha Mikel Arteta anamtaka Sesko kuwa usajili wake mkubwa kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, lakini Arsenal inakabiliwa na ugumu kukubaliana na mshahara anaotaka alipwe staa huyo.

Mawakala wa Sesko wanatafuta timu itakayompa mteja wao mshahara anaotaka tofauti na ofa iliyowekwa mezani na Arsenal kwa ajili ya kunasa saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.

Gyokeres ni chaguo mbadala la Arsenal, huku straika huyo wa Sweden akiwa tayari kuhama Sporting baada ya kuonyesha kiwango bora cha kufunga katika kikosi hicho cha wababe wa Ureno.

Straika Gyokeres anataka kuhamia kwenye Ligi Kuu England katika  dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini anafahamu kwamba yeye ni chaguo la pili huko Emirates.

Arsenal bado haijakamilisha dili la yeyote hapo, hivyo wote wawili bado wapo kwenye mipango ya kocha Arteta kwa ajili ya msimu ujao. Nani anafaa kuja Emirates dirisha hili?

USAJ 02

Mavitu ya Benjamin

Sesko 2024/25

Umri: Miaka 22

Klabu: RB Leipzig

Mechi: 45

Mabao: 21

Asisti: 6

Sesko anatazamwa kama moja ya mastraika vijana wanaoibukia kwa kasi ambao wanaweza kuja kuwa kitu kikubwa sana kwenye soka la dunia kwa siku za baadaye.

Hilo linabebwa na takwimu za straika huyo, ambapo kwa msimu uliopita, alihusika kwenye mabao 27, akifunga 21 na kuasisti sita katika mechi 45.

Alifunga mabao sita zaidi ya wakali wa Arsenal. Na anacheza kwenye ligi ngumu ya Bundesliga, ukilinganisha na ile ya Ureno anayocheza Gyokeres. Kwenye Bundesliga, Sesko amefunga mabao 13 tu, lakini kimo chake cha futi 6 na inchi 5 ndicho kitu kinacholeta imani kubwa kwamba atakwenda kufiti vyema katika mtindo wa Arteta.

USAJ 01

Mavitu ya Viktor

Gyokeres 2024/24

Umri: Miaka 27

Klabu: Sporting Lisbon

Mechi: 52

Mabao: 54

Asisti: 13

Kama Sesko bado hajakamilika vyema, basi Viktor Gyokeres ni mtambo halisi wa mabao. Staa huyo wa kimataifa wa Sweden, alifunga mabao 54 katika mechi 52 alizochezea Sporting msimu uliopita na kuliweka jina lake kwenye orodha ya washambuliaji wa kutisha Ulaya. Kwenye ligi, Gyokeres alifunga mara 39 katika mechi 33 na kuasisti mara saba.

Hata hivyo, kwenye mabao hayo 39 aliyofunga kwenye ligi, karibu theluthi moja ni ya penalti, akifunga mara 12. Si mrefu sana ukimlinganisha na Sesko, Gyokeres ana futi 6 na inchi 2, lakini imejengeka vyema kimwili na kuwa tishio ndani ya boksi kama ilivyo kwa Sesko.

Lakini, kinachowapasua kichwa mabosi wa Arsenal kwenye machaguo hayo ni tofauti ya umri wa wakali hao, mmoja bado mdogo na mwingine anaelekea kwenye kilele cha soka lake, huku wakiwaza kwamba usajili wao wa mchezaji wa kutoka Ureno basi uwe kama wa Bruno Fernandes huko Manchester United na usiwe kama wa Darwin Nunez huko Liverpool.