Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali ya pili kwa nyota Hull City

AJALI Pict

Muktasari:

  • Picha zilizosambaa mitandaoni zilionyesha gari likiwa limepinduka kwenye barabara nyembamba ya Millhouse Woods Lane, inayokwenda kwenye kituo cha mazoezi cha Hull City kilichopo Cottingham. Inadaiwa kwamba hiyo ni ajali ya pili kwa mchezaji wa Hull City ndani ya siku chache. Picha hizo zilionyesha gari aina ya Mercedes likiwa limepinduka, huku taarifa kamili kuhusu tukio hilo hadi jana mchana zilikuwa hazijawekwa wazi.

COTTINGHAM, ENGLAND: NYOTA wa Ligi Kuu England, Lucas Gourna-Douath, amepata ajali na gari lake kugeukia nje ya uwanja wa mazoezi wa timu yake, Hull City, kabla ya kutoka kwenye tukio hilo bila majeraha.

Picha zilizosambaa mitandaoni zilionyesha gari likiwa limepinduka kwenye barabara nyembamba ya Millhouse Woods Lane, inayokwenda kwenye kituo cha mazoezi cha Hull City kilichopo Cottingham. Inadaiwa kwamba hiyo ni ajali ya pili kwa mchezaji wa Hull City ndani ya siku chache. Picha hizo zilionyesha gari aina ya Mercedes likiwa limepinduka, huku taarifa kamili kuhusu tukio hilo hadi jana mchana zilikuwa hazijawekwa wazi.

Licha ya klabu hiyo kuwa haijatoa uthibitisho rasmi, mtandao dada wa Daily Star Sport, Hull Live, unaamini gari hilo ni la Gourna-Douath aliyesajiliwa na klabu hiyo kwa ada ya Pauni 3.4 milioni katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, na ndiye aliyekuwa akiendesha, lakini  amenusurika kwenye tukio hilo bila majeraha.

AJA 01

Hiyo ni mara ya pili ndani ya wiki chache kwa mchezaji wa Hull City kupata ajali na gari lake kuziba kwa muda barabara hiyo, kwani Septemba 11 mwaka huu, winga mpya Sorba Thomas aliyesajiliwa kwa Pauni 10.5 milioni alinusurika bila majeraha baada ya gari lake kupinduka miguu juu paa chini.

Baada ya ajali iliyohusisha Land Rover Defender ya Sorba yenye thamani ya Pauni 60,000 mwezi uliopita, ambapo mmoja wa wafanyakazi wa klabu hiyo anayeaminika kuwa kocha Sergej Jakirovic, alikuwepo eneo la tukio, ujumbe wa usalama ulitolewa.

Phil Redshaw, diwani wa eneo hilo alitoa taarifa akifichua kwamba alikuwa amewasiliana na klabu hiyo kuhusu umuhimu wa wachezaji kuwa waangalifu wanapokaribia kituo cha mazoezi.

AJA 02

Amesema: “Nilimwandikia katibu wa Klabu ya Hull City nikiomba awakumbushe wachezaji kuwa waangalifu wanapoendesha magari kwenye barabara hiyo kutokana na wasiwasi wa wakazi. Nilitaka awakumbushe wafanyakazi wao kuendesha kwa uangalifu zaidi, kwa sababu kila msimu wanasajili wachezaji wapya.”

Millhouse Woods Lane ni barabara nyembamba inayoelekea kwenye kituo cha mazoezi cha klabu hiyo, ikiwa na nafasi ndogo kwa magari kupishana, kwa mujibu wa Hull Live. Kutokana na hali hiyo, awali kulikuwa na tahadhari zilizotolewa kuhusu mwendo ambao baadhi ya magari yamekuwa yakiendeshwa wakati yakipita katika sehemu hiyo finyu.

Gourna-Douath, kama ilivyo kwa Thomas, alijiunga na Hull City iliyopanda daraja msimu huu akitokea Red Bull Salzburg, ambapo kiungo huyo Mfaransa amecheza mechi tatu, lakini ameanza katika kikosi cha kwanza mara moja.