Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aibu FIFA Kombe la Dunia viti kibao vikibaki wazi

Mexico City, Mexico. IDADI kubwa ya viti visivyo na watu ilionekana wakati Korea Kusini ilipogeuza matokeo na kuifunga Czech katika mechi ya pili ya Kombe la Dunia iliyopigwa jana, katika tukio lililobua mjadala mkubwa kuhusu mfumo wa uuzaji tiketi uliowekwa na Fifa kuelekea mashindano hayo.

Mkakati huo wenye utata wa Fifa ulionekana wazi kwa watazamaji wa televisheni duniani kote tangu siku ya kwanza ya mashindano, ambapo mapema siku hiyo kituo cha FOX kilikiuka kanuni za Fifa kwa kuonyesha matangazo wakati wa mapumziko ya kunywa maji na kukatiza matangazo ya moja kwa moja ya mechi ya ufunguzi.

Mechi ya pili ya mashindano iliyowakutanisha Korea Kusini na Czech kwenye Uwanja wa Estadio Akron mjini Guadalajara, ilitoa ishara ya wazi ya tatizo hilo kwani sehemu nyingi za viti zilionekana tupu katika mchezo, hasa maeneo ya VIP na sehemu zilizokuwa mbali na kamera za televisheni.

Hali hiyo ilifuatia sintofahamu iliyoshuhudiwa katika mchezo wa kwanza wa mashindano. Ni jambo ambalo Fifa ilikuwa imetumia miezi kadhaa na mamilioni ya dola kujaribu kulizuia. Hata mwanzoni mwa mwezi Juni, shirikisho hilo lilipunguza kimyakimya bei za tiketi kwa mechi zote 104 za mashindano na kuachia asilimia 70 ya vyumba vya hoteli vilivyokuwa vimehifadhiwa kwa wingi, katika kile kilichoonekana kuwa juhudi za mwisho za kujaza viwanja.

Kabla ya kuanza kwa mashindano, takribani tiketi 180,000 zilikuwa bado hazijauzwa kupitia majukwaa rasmi ya Fifa ya mauzo ya pili. Takribani tiketi 15,000 za hatua ya makundi zilikuwa bado zinapatikana moja kwa moja kupitia tovuti ya shirikisho hilo. Kwa mechi ya ufunguzi ya Marekani dhidi ya Paraguay iliyopigwa jana Juni 12, zaidi ya tiketi 4,400 zilikuwa bado hazijanunuliwa kupitia njia rasmi.

Tiketi za bei nafuu zaidi zilikuwa zikiuzwa kwa Dola 1,120 (zaidi ya Sh 2.8 milioni) moja kwa moja kutoka Fifa, huku wastani wa bei katika soko la mauzo ya pili ukiwa zaidi ya Dola 800 (tariban Sh2.2), hata baada ya kushuka kwa asilimia 20 katika mwezi uliopita.

Chanzo kikuu cha sintifahamu kinatajwa kuwa uamuzi wa Fifa kutumia mfumo wa bei zinazobadilika kulingana na mahitaji kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia. Ingawa imekuwa ikijitahidi kutofautisha mfumo huo, wakosoaji wengi wanaona tofauti hiyo ni ya maneno.

Bei za tiketi kwa mechi 90 kati ya 104 zilipanda kwa wastani wa asilimia 34 kati ya Oktoba 2025 na Aprili 2026.

Hata hivyo, rais wa Fifa, Gianni Infantino, alitetea sera hiyo katika mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari akisema: “Kama tungeuza tiketi kwa bei ya chini zaidi katika soko hili maalumu zingekwenda kwenye soko la pili kwa bei kubwa zaidi, jambo ambalo si halali. Fedha hizo zingeishia kwa waendeshaji wa masoko ya pili au biashara haramu badala ya kuingia kwenye mpira wa miguu.”

Aliongeza: “Kuhusu uchunguzi wa kisheria na malalamiko yaliyowasilishwa katika baadhi ya majimbo ya Marekani hatuna wasiwasi wowote. Kabla ya kuanza kuuza tiketi milioni 6.5 hadi milioni saba, tulishauriana na mawakili na wataalamu bora. Kama tumefanya kosa, basi ina maana kila anayejihusisha na uuzaji wa tiketi Amerika Kaskazini anafanya kosa pia.”

Mawakili wa majimbo ya New York na New Jersey, Marekani wameanzisha uchunguzi kuhusu mfumo huo wa bei, na wametuma wito kwa Fifa kutoa maelezo, huku baadhi ya wabunge wa Marekani pia wakimtaka Infantino kufika mbele yao ili kutoa ufafanuzi.

Siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano, Infantino alisisitiza kuwa bei hizo zilikuwa muhimu ili kuzuia tiketi kutouzwa kwa magendo katika soko la pili. Hata hivyo, viti tupu vilivyoonekana siku ya ufunguzi vinaonekana kuwa jibu zaidi dhidi ya hoja hiyo. Fifa ilikuwa ikitamba kwamba tovuti yake ya tiketi ilikuwa imepokea zaidi ya maombi milioni 500. Lakini kutokana na picha zilizoonekana katika mechi za ufunguzi inaonekana kwamba mahitaji ya tiketi kwa bei zilizowekwa na Fifa yalikuwa madogo zaidi kuliko ilivyotarajiwa.