Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Adidas yazindua uzi wa mwisho wa Messi

Muktasari:

  • Argentina, Scotland na mataifa mengine yamepata uzi wenye mwonekano wa ‘retro’ wenye nembo ya zamani ya Trefoil ambao uliwahi kuwa maarufu miaka ya zamani.

BONN, UJERUMANI: KAMPUNI ya vifaa vya michezo ya Adidas imezindua rasmi jezi za mwisho za Kombe la Dunia 2026 za nchji mbalimbali ikiwamo ya Argentina ambapo supastaa Lionel Messi anatarajiwa kuichezea kwa mara ya mwisho katika mashindano.

Argentina, Scotland na mataifa mengine yamepata uzi wenye mwonekano wa ‘retro’ wenye nembo ya zamani ya Trefoil ambao uliwahi kuwa maarufu miaka ya zamani.

Huku hesabu ya kuelekea Kombe la Dunia 2026 zikiendelea kwa nchi mbalimbali zikiwa zimebaki chini ya siku 84, uzinduzi wa jezi umekuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya fainali za mashindano makubwa ya fainali za mabara au dunia.

Mashindano hayo yatafanyika Marekani, Mexico na Canada, huku mataifa makubwa kama Argentina, Ujerumani na Hispania yakilenga kutwaa taji kutokana na kuwa na vikosi vilivyojaa mastaa wadogo ambao wanakiwasha vilivyo kwenye klabu wanazozichezea.

Tofauti kubwa safari hii ipo kwenye jezi, ambapo Adidas imerudisha nembo yake maarufu ya Trefoil kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36. Muundo huo wa jezi umechochewa na mtindo wa miaka ya 1990 na utavaliwa na nyota kama Lionel Messi, Lamine Yamal (Hispania), Scott McTominay (Scotland) na Florian Wirtz (Ujerumani).


Kombe la Dunia la mwisho kwa Messi?

Kwa sasa kinachozungumzwa ni iwapo nyota huyo na mshindi wa Ballon D’or mara nane ikiwa ni zaidi ya mchezaji yeyote duniani iwapo atamalizana na timu ya taifa lake akiwa bingwa tena baada ya kubeba nchini Qatar 2022.

Messi anatarajiwa kuiongoza Argentina kama nahodha katika Kombe la Dunia la mwisho, akilenga kuongeza taji lingine baada ya ushindi wa 2022 dhidi ya Ufaransa, ambapo alimtangulia tena kwa mafanikio mshindani wake uwanjani, Cristiano Ronaldo.


Hispania na wengine

Hispania ina kikosi bora kikiongozwa na vipaji kama Yamal, na inaonekana kuwa mojawapo wa timu zinazopigiwa upatu kushinda tena taji la dunia kwa mara ya kwanza tangu 2010 ilipobeba kupitia fainali zilizopigwa Afrika Kusini zikiwa ni pekee Afrika.

Kwa upande mwingine, Scotland imekuwa ikivutia macho kwa jezi yake ya ugenini yenye rangi ya kipekee inayofanana na “Irn-Bru”, huku Ujerumani nayo ikionekana kuwa mshindani mkubwa uwanjani na hata kwenye ubora wa jezi.

Aidha, mataifa kama Colombia, Ubelgiji, Italia, Wales na wenyeji Mexico pia yamepata mwonekano huo wa retro.

Kwa ujumla, Kombe la Dunia 2026 linatarajiwa kuwa bora zaidi kihistoria, na pia moja ya mashindano yenye jezi zenye mvuto zaidi kuwahi kuonekana.