Adebayor ainyima ubingwa Arsenal, ataja sababu za kuipa Man City
Muktasari:
- Adebayor amezungumza na Premier League Productions baada ya ushindi wa Arsenal, akisisitiza Manchester City ina mechi moja mkononi ikilinganishwa na The Gunners, jambo ambalo linaweza kuwa faida kwa kikosi cha Pep Guardiola.
ALIYEKUWA nahodha na mshambuliaji timu ya taifa ya Togo, Emmanuel Adebayor, amesisitiza kuwa Manchester City itaibuka bingwa wa taji la Ligi Kuu ya England msimu huu, licha ya Arsenal kuongoza kwa tofauti ya pointi tano baada ya kuichapa Tottenham Hotspur mabao 4‑1, jana Jumapili, Februari 22, 2026.
Adebayor amezungumza na Premier League Productions baada ya ushindi wa Arsenal, akisisitiza Manchester City ina mechi moja mkononi ikilinganishwa na The Gunners, jambo ambalo linaweza kuwa faida kwa kikosi cha Pep Guardiola.
“Nimeangalia ratiba zinazofuata kwa Arsenal na City. Nafikiri City ndiyo itashinda taji la EPL msimu huu,” amesema Adebayor.
“Mimi nategemea zaidi uzoefu wa City. Guardiola ameshawahi kushinda ligi hii na ana wachezaji waliopata taji hilo pia. Aidha, amejumuisha wachezaji wapya katika kikosi chake.
“Arsenal wameonyesha kitu na dhamira katika mechi dhidi ya Spurs, lakini je, wanaweza kufanya hivyo katika mechi 10 zilizobaki? Nina shaka,” amesema.
Kauli ya Adebayor inalingana na dhana ya wengi kuwa Manchester City, chini ya uzoefu wa Guardiola na wachezaji wake waliokuwa washindi wa ligi hapo awali, wana nafasi kubwa ya kuondoka na taji msimu huu, huku Arsenal ikihitaji umakini mkubwa ili kudumisha nafasi yao ya kuiongoza ligi hadi mwisho wa msimu huu.
Mechi za Arsenal zilizobaki
Arsenal vs Chelsea (nyumbani)
Brighton vs Arsenal (ugenini)
Arsenal vs Everton (nyumbani)
Bournemouth vs Arsenal (ugenini)
Manchester City vs Arsenal (ugenini)
Arsenal vs Newcastle (nyumbani)
Arsenal vs Fulham (nyumbani)
West Ham vs Arsenal (ugenini)
Arsenal vs Burnley (nyumbani)
Crystal Palace vs Arsenal (ugenini)
Mechi za Man City zilizobaki
Leeds vs Man City (ugenini)
Man City vs Nottingham Forest (nyumbani)
West Ham vs Man City (ugenini)
Chelsea vs Man City (ugenini)
Man City vs Crystal Palace (nyumbani)
Man City Arsenal (nyumbani)
Burnley vs Man City (ugenini)
Everton vs Man City (ugenini)
Man City vs Brentford (nyumbani)
Bournemouth vs Man City (ugenini)
Man City vs Aston Villa (nyumbani)