Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ada kubwa ya usajili wa wachezaji byebye!

ADA Pict

Muktasari:

  • Chama cha kimataifa cha wachezaji wa kulipwa (FifPro) kinaishutumu Fifa kwa kuwa kikwazo kwenye sheria mpya ya uhamisho wa wachezaji baada ya Makahama ya Ulaya kukubali kwamba staa wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Lassana Diarra alishikiliwa kimakosa na timu ya Lokomotiv Moscow ya Russia muongo mmoja uliopita.

LONDON, ENGLAND: ISHU ya wanasoka mastaa kusajiliwa kwa pesa nyingi inaweza kuwa historia baada ya mabosi wanaowasimamia wachezaji hao kutaka mastaa kuwa na uhuru wa kuvunja mikataba yao kwa kulipa fidia wanapoona inatosha kucheza timu moja na kuamua kuhamia kwingine.

Chama cha kimataifa cha wachezaji wa kulipwa (FifPro) kinaishutumu Fifa kwa kuwa kikwazo kwenye sheria mpya ya uhamisho wa wachezaji baada ya Makahama ya Ulaya kukubali kwamba staa wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Lassana Diarra alishikiliwa kimakosa na timu ya Lokomotiv Moscow ya Russia muongo mmoja uliopita.

Wakala mahiri wa wanasoka walidai hukumu hiyo ya Oktoba mwaka jana ilikuwa hatua moja muhimu kuelekea kwenye mtindo wa Marekani wa wachezaji kuwa huru, kitu ambacho ishu ya kulipiwa ada kinakuwa kimepitwa na wakati, ambapo wachezaji sasa watakuwa wanalipa fidia tu ya sehemu ya mikataba yao iliyobaki ili kuhama timu.

Klabu vigogo na Fifa wanapambana kupinga hatua hiyo, wakati huu klabu za Ligi Kuu England tayari zikiwa zimeshatumia Pauni 375 milioni kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Lakini, FifPro sasa imewaambia wachezaji pamoja na wanasheria wao kujiandaa kuibana Fifa kwa kushindwa kulazimisha utendaji kazi wa sheria ya Ulaya ili kuwapo na uhuru kwenye kuhama.

Mkuu wa sheria wa FifPro, Alexandra Gomez Bruinewoud alisema: “Kila mfanyakazi anapaswa kuwa na haki ya kusitisha uhusiano wake wa kimkataba. Kufahamu ni kiasi gani unachopaswa kulipa fidia hiyo ni sehemu ya haki.

“Pia, kuondoka kazini kwako isikuzuie kwenda kuajiriwa kwenye kazi nyingine, kama ambavyo inatokea kwenye soka.”€

Jambo hilo linafanya vigogo wa soka sasa kukuna vichwa kutokana na kile kilichoamriwa Moscow miaka 10 iliyopita.

Kiungo wa zamani wa Chelsea, Arsenal na Portsmouth, Diarra pengine hakuwa na maajabu sana kwenye Ligi Kuu England alikocheza kwa misimu mingi, akitumika kwenye mechi 44, lakini ushindi wa kesi yake unaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye soka la Ulaya na duniani kote linapokuja suala la uhamisho wa wachezaji. Na kwa ushindi huo wa Diarra unaifanya FifPro kuingia na kuona kuna umuhimu wa wachezaji kuwa na haki ya kuvunja mikataba.

Kutokana na hilo, ishu za mchezaji kusajiliwa kwa ada ya uhamisho inaweza kufutwa kabisa, kitu ambacho kinaweza kusababisha wachezaji wenye thamani ya Pauni 100 milioni kwa sasa, kupatikana sokoni kwa pesa ndogo.

Hata hivyo, sheria hiyo mpya inaweza isitumike kwenye dirisha hili. Lakini, msimamo wa FifPro ni kuhakikisha hilo linatimia ili kwenda sambamba na sheria za Ulaya. Na sasa wachezaji mahiri waliokuwa wakinufaika na kulipwa mishahara mikubwa na kusajiliwa kwa mikataba mirefu, wanaweza kujikuta akilipwa pesa kiduchu na mikataba mifupi. Sakata hilo linaweza kuibukia kwenye ile kesi ya Jean-Marc Bosman, aliyeshinda ishu ya mchezaji kuwa huru na kujiunga na timu yoyote anayotaka hata kama usajili umeshafungwa.