Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ada kikwazo uhamisho wa Darwin Nunez kwa Napoli

TETESI Pict

Muktasari:

  • Nunez mwenye umri wa miaka 26, anadaiwa kuwa hamfurahishi sana kocha Arne Slot ambaye anahitaji huduma ya mshambuliaji mwingine kwani anaona kuwa yeye hatoshi.

STRAIKA wa Liverpool, Darwin Nunez yuko tayari kujiunga na Napoli katika dirisha hili la majira  ya kiangazi, lakini changamoto kubwa inayokwamisha dili hilo ni Napoli kutokuwa tayari kutoa pauni 70 milioni inayohitajika na Liverpool.

Nunez mwenye umri wa miaka 26, anadaiwa kuwa hamfurahishi sana kocha Arne Slot ambaye anahitaji huduma ya mshambuliaji mwingine kwani anaona kuwa yeye hatoshi.

Staa huyu wa kimataifa wa Uruguay katika msimu uliopita alicheza mechi 47 za michuano yote na kufunga mabao saba.

Mkataba wa sasa wa Nunez unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, mbali ya Napoli, huduma yake pia inawindwa na Juventus na baadhi ya timu za Saudi Arabia.


Emiliano Martinez

CHELSEA imepewa nafasi ya kumsajili kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez kwa pauni 45 milioni katika dirisha hili la majira ya kiangazi lakini Martinez wenyewe anaonekana kuwa na nia zaidi ya kujiunga na Manchester United badala ya matajiri hao wa Jiji la London.

Mkataba wa Martinez na Villa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, lakini kipa huyu ameomba kuondoka.


Jarell Quansah

BEKI wa Liverpool na England, Jarell Quansah mwenye umri wa miaka 22, atafanyiwa vipimo vya afya Bayer Leverkusen leo, Jumatatu kabla ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na timu hiyo kwa pauni 35 milioni katika dirisha hili.

Quansah ni miongoni mwa mastaa ambao wameomba kuondoka Liverpool katika dirisha hili ili kupata muda mwingi zaidi wa kucheza.


Marc Guehi

LIVERPOOL iko karibu kufanikisha dili la kumsajili beki wa kati wa Crystal Palace na England mwenye umri wa miaka 24, Marc Guehi katika dirisha hili.

Inaelezwa hadi sasa majogoo hawa wameshafikia makubaliano binafsi na mchezaji mwenyewe na wapo katika hatua za mwisho kukabiliana na Palace wenyewe kabla ya kukamilisha dili hilo.


Habib Diarra

SUNDERLAND imekubali kutoa pauni 30 milioni kwa ajili ya kukamilisha usajili wa kiungo wa Strasbourg na timu ya taifa ya Senegal mwenye umri wa miaka 21, Habib Diarra katika dirisha hili.

Diarra ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, msimu uliomalizika alicheza mechi 33 za michuano yote na kufunga mabao manne.


Tyler Dibling

TAARIFA zinaeleza Crystal Palace iko tayari kushindana na Newcastle, Liverpool na Tottenham katika vita ya kuiwania saini ya winga wa Southampton, Tyler Dibling mwenye umri wa miaka 19, katika dirisha hili. Dibling amekuwa katika rada za timu nyingi England tangu dirisha la majira ya baridi mwaka huu kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika dirisha lililopita.


James Trafford

HADI sasa Newcastle bado inapambana kwa ajili ya kumsajili kipa wa Burnley, James Trafford katika dirisha hili baada ya ofa yao ya awali ya pauni 25 milioni kukataliwa.

Ripoti zinaeleza, Newcastle imeshafanya makubaliano binafsi na staa huyu na sasa inapambana kufikia makubaliano na Burnley kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.


Jhon Duran

AL-NASSR tayari imekubali kumpeleka kwa mkopo kwenda Fenerbahce mshambuliaji wao raia wa Colombia, Jhon Duran mwenye umri wa miaka 21, katika dirisha hili. Ripoti zinadai Duran ameomba kutolewa kwa mkopo ili kurudi tena Ulaya na kucheza michuano ya kimataifa na kuna uwezekano akasaini mkataba wa kudumu baada ya msimu mmoja.