Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AC Milan yawekeza nguvu dili la Darwin Nunez

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Nunez anahusishwa kuondoka baada ya mabosi wa Liverpool kumpa ruhusa ya kutafuta timu mpya kwani inahitaji kusajili mshambuliaji mwingine.

AC Milan iko kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Liverpool, Darwin Nunez, 26, ili kumsajili dirisha hili la majira ya kiangazi.

Licha ya nia yao juu ya Nunez ripoti zinadai Milan inakumbana na ushindani wa kutoka kwa Al Hilal ya Saudi Arabia ambayo pia inahitaji saini yake.

Nunez anahusishwa kuondoka baada ya mabosi wa Liverpool kumpa ruhusa ya kutafuta timu mpya kwani inahitaji kusajili mshambuliaji mwingine.

Mbali ya staa huyu Milan pia inaangalia uwezekano wa kuwasajili Dusan Vlahovic kutoka Juventus pamoaja  na Rasmus Hojlund lakini kwa sasa kipaumbele ni Nunez.

Nunez amekuwa akitajwa kuondoka sana Anfield kwa sasa kutokana na  ujio wa Hugo Ekitike na Florian Wirtz unaonekana kumshusha zaidi kwenye orodha ya wachezaji wanaopewa kipaumbele na kocha Arne Slot.

Vilevile Liverpool bado wanaonyesha nia ya kumsajili nyota wa Newcastle, Alexander Isak na ikiwa itafanikisha hilo, nafasi ya Nunez katika kikosi cha kwanz aitakuwa finyu sana.

Hapo awali fundi huyu alikuwa akiwindwa na Napoli ambayo kwa sasa imeelekeza juhudi zao kwingine baada ya kushindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Liverpool katika masuala ya ada ya uhamisho.

Baada ya kumkosa Nunez, Antonio Conte aliendekeza jina  mshambuliaji wa Udinese, Lorenze Lucca ambaye amesajiliwa kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua mazima kwa dau la Euro 26 milioni.



Callum Brittain

DILI la beki wa Blackburn,  Callum Brittain, mwenye miaka 27,  kusajiliwa na Middlesbrough  katika dirisha hili linadaiwa kukwama kutokana na masuala ya ada ya uhamisho. Katika makubaliano ya awali Middlesbrough ilipanga kutoa Pauni 3.5 milioni kama  ada ya  uhamisho ya  Callum lakini Blackburn inaripotiwa kuhitaji zaidi. Mkataba wa sasa wa Brittain unatarajiwa kumalizika mwakani. Msimu uliopita akiwa na Blackburn  alicheza mechi 35 za michuano yote na kufunga mabao mawili.


Tyler Morton

LIVERPOOL inahitaji Pauni 15 milioni kutoka kwa Olympique Lyon  ili kumuuza kiungo wao raia wa England,  Tyler Morton, mwenye umri wa  miaka 22 katika dirisha hili. Ripoti zinadai, Swawakilishi wa Lyon waliwasili  England tangu wiki iliyopita kwa ajili ya kumalizia hatua ya mwisho ya mazungumzo kabla ya kumsajili staa huyo. Morton hakuwa anapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Liverpool na awali alihitaji kuondoka hata kwa mkopo.


Randal Kolo Muani

TOTTENHAM , Manchester United na Newcastle zinafuatilia kwa karibu mustakabali wa mshambuliaji wa Paris St-Germain, Randal Kolo Muani, mwenye umri wa miaka 26, baada ya mpango wake wa kujiunga na Juventus kukwama. Timu hizi zinahitaji sana huduma ya fundi huyu wa kimataifa wa Ufaransa ili kuboresha maeneo yao ya ushambuliaji. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Fabio Silva

MABOSI wa Wolves wanahitaji zaidi ya Pauni 30 milioni kutoka kwa AS Roma inayohiraji kumsajili mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ureno, Fabio Silva, 23, katika dirisha hili. Taarifa kutoka Skysports, zinaeleza kuwa wawakilishi wa AS Roma wameshawasili England kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya hatua yapili kwa ajili ya wachezaji hao. Mbali ya Silva, Roma pia inawasiliana na Manchester City kwa ajili ya kumsajili  winga wa klabu hiyo.


Max Alleyne

WATFORD bado inafanya mazungumzo na  Manchester City kwa ajili ya kuipaya saini ya beki kisiki wa klabu hiyo na England, Max Alleyne  ambaye inahitaji kumsajili katika dirisha hili la majira ya kiangazi. Staa huyu mwenye umri wa miaka 20, ni miongoni mwa wachezaji ambao hawana nafasi katika kikosi cha kwanza cha Man City na msimu uliopita. Msimu uliopita alicheza  mechi 28 za michuano yote, alifunga bao moja.


Leo Castledine

KIUNGO wa Chelsea na timu ya taifa ya England chini ya miaka 19, Leo Castledine, 19, anatarajiwa kujiunga na Huddersfield Town kwa mkopo wa msimu mmoja katika dirisha hili. Castledine ambaye msimu uliopita alicheza mechi  27 za michuano yote na kufunga mabao mawili, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Rob Holding

Beki kisiki wa England Rob Holding ambaye kwa sasa yupo huru baada ya mkataba wake na Crystal Palace, kumalizika, anatarajiwa kujiunga na  Colorado Rapids inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani, dirisha hili la majira ya kiangazi. Kabla ya kufikia makubaliano ya kumsajili staa huyu Colorado ilikuwa katika vita kali dhidi ya Sheffield United na Wrexham ambazo pia zilimhitaji.

Msimu uliopita alicheza mechi 18 za michuano yote.