Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya Mourinho apelekwa mchangani Kombe la FA

Haya Mourinho apelekwa mchangani Kombe la FA

Muktasari:

KOMBE la FA lina raha yake. Timu ya mchangani ya Marine imetinga hatua ya tatu ya Kombe la FA na kupata fursa ya kukipiga dhidi ya Tottenham Hotspur ya Jose Mourinho kwenye uwanja wao wa nyumbani.

LONDON, ENGLAND. KOMBE la FA lina raha yake. Timu ya mchangani ya Marine imetinga hatua ya tatu ya Kombe la FA na kupata fursa ya kukipiga dhidi ya Tottenham Hotspur ya Jose Mourinho kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Marine inakuwa timu ya pili kwa timu za mchangani kufika kwenye hatua hiyo baada ya kuwasukuma nje timu ya League Two, Colchester kwa mikwaju ya penalti, Havant na Waterlooville. Mechi hiyo ni kitu kizuri kwa Niall Cummins, mfungaji wao wa bao la ushindi kwenye raundi ya pili, ambaye ni shabiki wa mahasimu wa Spurs, Arsenal.

Sasa watakuwa nyumbani kwenye uwanja wao unaoingiza watazamaji 3,185 huko Merseyside kuwakaribisha vinara hao wa Ligi Kuu England msimu huu. Kutakuwa na mashabiki wachache watakaoruhusiwa kutazama mechi hiyo. Mechi hiyo itashuhudia timu mbili zilizotofautiana sana kumenyana kwenye raundi ya tatu.

Kocha Neil Young alisema: “Hii ni droo ya aina yake. Tumecheza mechi saba hadi kufikia hapa, ni zawadi kubwa. Kwa wachezaji wetu, kamati na mashabiki kutufikisha hapa, ni aina yake kwetu.”

Wachezaji wa Morecambe wanafurahia pia kupangwa na Chelsea na watakwenda kukipiga Stamford Bridge. Huko kwingineko, Manchester United watawakaribisha Watford nyumbani Old Trafford, wakati mabingwa watetezi Arsenal watakipiga na Newcastle United katika mechi ya wababe watupu wa Ligi Kuu England.

Liverpool watasafiri kuwafuata Aston Villa, bila shaka wataogopa kisijirudie kichapo cha mabao 7-2 walichokumbana nazo kwenye ligi na Manchester City watakipiga na Birmingham.

Mechi za hatua hiyo ya raundi ya tatu zitapigwa wikiendi Januari 9 na 10 mwakani.

MECHI ZENYEWE ZA RAUNDI YA TATU

-Huddersfield v Plymouth

-Southampton v Shrewsbury

-Chorley v Derby

-Marine v Tottenham

-Wolves v Crystal Palace

-Stockport County v West Ham

-Oldham Athletic v Bournemouth

-Man United v Watford

-Stevenage v Swansea City

-Everton v Rotherham

-Nott.Forest v Cardiff City

-Arsenal v Newcastle

-Barnsley v Tranmere Rovers

-Bristol Rovers v Sheffield Utd

-Canvey Island/Boreham Wood v Millwall

-Blackburn v Doncaster

-Stoke City v Leicester City

-Wycombe v Preston

-Crawley Town v Leeds United

-Burnley v MK Dons

-Bristol City v Portsmouth

-QPR v Fulham

-Aston Villa v Liverpool

-Brentford v Middlesbrough

-Man City v Birmingham City

-Luton Town v Reading

-Chelsea v Morecambe

-Exeter City v Sheffield Wed

-Norwich City v Coventry City

-Blackpool v West Brom

-Newport County v Brighton

-Cheltenham Town v Mansfield Town