Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pique aonekana Shakira akitumbuiza

TUZ 01

Muktasari:

  • Beki wa zamani wa Barcelona na Hispania, Gerard Pique, alionekana akiwasili katika Uwanja wa New York/New Jersey akiwa ameongozana na watoto wake, jambo lililovuta hisia za mashabiki.

DALLAS, MAREKANI: FAINALI za Kombe la Dunia 2026 kati ya Hispania na Argentina haikuanza kwa kipenga cha mwamuzi pekee, bali ilianza kwa gumzo lililoibuka saa kadhaa kabla ya mechi.

Beki wa zamani wa Barcelona na Hispania, Gerard Pique, alionekana akiwasili katika Uwanja wa New York/New Jersey akiwa ameongozana na watoto wake, jambo lililovuta hisia za mashabiki.

Kilichowashangaza wengi ni Pique aliingia kupitia njia za kawaida pamoja na maelfu ya mashabiki, badala ya kutumia lango maalumu la wageni mashuhuri kama ilivyotarajiwa. Picha na video zake zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuwa miongoni mwa gumzo kubwa kabla ya mchezo kuanza.

Baadaye, Pique alikaa jukwaani kushuhudia Hispania ikiifunga Argentina na kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya pili katika historia yake.

PIQ 02

Shakira avuta macho zaidi

Hata hivyo, tukio lililokuwa likisubiriwa kwa hamu zaidi lilikuwa burudani ya mapumziko ya kipindi cha kwanza.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia, FIFA iliandaa Halftime Show kwenye fainali, huku mwanamuziki maarufu Shakira akiwa mmoja wa wasanii wakuu waliotumbuiza.

Wakati burudani hiyo ikiendelea, video nyingine iliyorekodiwa kutoka jukwaani ilianza kusambaa mtandaoni.

Video hiyo iliwaonyesha watoto wa Pique wakifurahia kwa shangwe maonyesho ya Shakira, huku Pique mwenyewe akionekana mtulivu na mwenye sura ya kutafakari kwa muda katika sehemu kadhaa za onesho hilo.

PIQ 01

Mitandao yachangamka

Taswira hiyo ilitosha kuibua maelfu ya maoni kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Wengi waliona ni tukio la kipekee kumwona Pique akiwa uwanjani wakati aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Shakira, akifanya moja ya maonyesho makubwa zaidi katika historia ya soka mbele ya mamilioni ya watazamaji duniani.

Ingawa hakukuwa na mawasiliano yoyote kati yao yaliyoonekana hadharani, uwepo wa wawili hao katika tukio hilo uligeuka kuwa moja ya simulizi zilizotawala mijadala ya fainali.

Mbali na ushindi wa Hispania dhidi ya Argentina, fainali hiyo itaendelea kukumbukwa kwa burudani ya kihistoria ya Shakira pamoja na picha za Pique na watoto wake zilizozua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki duniani.