Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazito FC waachilia majembe sita

Siku moja tu baada ya dirisha Dogo la uhamisho la Ligi Kuu ya FKFPL kufungwa ,Wazito Fc kupitia kurasa zao za kijamii wametangaza rasmi kuondoka kwa wachezaji Sita kwenye timu Hiyo.
Timu Hiyo chini ya mkufunzi mpya Fred Ambani, anaendelea kunoa timu hii ilikuweza kujiondoa kwenye mtego wa kushuka daraja ,Kwani Wazito wanashikilia nafasi ya 15 na alama 16. Wachezaji waliondoka ni ;


Kevin Kimani
Alijunga na timu ya Wazito mwezi Septemba mwaka 2020 na kuisaidia Wazito kumaliza katika nafasi ya tisa na alama 45 Msimu jana chini ya Mkufunzi Francis Kimanzi. Baada ya kuwa kwenye timu hii kwa mwaka mmoja unusu sasa amejiunga na timu ya Bandari Fc .
Kimani baada ya kujiunga na timu hiyo  wiki jana, alicheza dhidi ya Tusker nyumbani Na ugenini Lakini Bandari wakalala mikononi mwa Tusker kwa bao 1-0 kwa mechi zote mbili.
Kimani anasema maamuzi ya kuondoka kwenye timu ya  Wazito aliyafanya kutokana na ofa ambazo alipata kutoka kwa timu tofauti ,lakini Bandari walikuwa na ofa nzuri zaidi.
‘Wazito walikuwa ni familia yangu lakini ulipofika wakati wa kuondoka nilifanya maamuzi mara moja, langu tu nikuwatakia kila la kheri kwa mechi zijazo . Niliamua kujiunga na timu tofauti mbali na mji mkuu Nairobi ,lakini mpira ni ule ule nitajituma kama kawaida  kuisaidia Bandari kuendele kufanya vizuri Ligi kuu .Bandari na wahakikishia mabao mengi msimu huu kutokana na uzoefu ninao wa timu ya taifa na Ligi kuu ninaimani nitakuwa na mchango mkubwa kwa timu ya Bandari hata ingawa tumepoteza hii leo bado tuna mda wakurekebisha .’Alisema Kimani
Mchezaji Huyo mwenye miaka 32 amewahi kuichezea klabu ya Mathare United,KCB ,Tusker ,Sofapaka,Bolcholter nchini Belgian ,Fostiras kutoka Greece ,Jomo Cosmos ya Africa Kusini ,AFC Leopards na Al-Hazem SC nchini Saudia.


Cliff Nyakeya
Alijiunga na timu ya Wazito Septemba mwaka  jana kutoka Masr ya Misri baada ya kuvunja mkataba wake wa miaka miwili na timu hiyo  .
Nyakeya,27, ambaye pia anaitumikia timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars ,tetesi zina Sema kuwa huenda  akajiunga na timu ya AFC Leopards.
Kiungo Huyu wakati amewahi kuichezea timu ya Gor Mahia  na Mathare United.

Vincent Oburu
Baada ya kuitumikia Wazito Fc kwa mwaka mmoja unusu,Oburu alijiunga rasmi na klabu ya Zesco United Ligi Kuu Zambia.
Oburu, 23, alijiunga na Wazito kutokea AFC Leopards baada ya kuchezea timu Hiyo kwa misimu minne. Pia, aliwahi kuchezea Green Heaven Fc,Shofco Fc na anachezea timu ya Taifa Harambee Stars.

Erick Gichimu
Tetesi zina Sema Gichimu amerudi nyumbani kwa timu ya Bidco United,hii  ni baada ya mambo kutomwendea alivyokuwa anatarajia kwenye timu ya Wazito na kuvunja mkataba wake.
Straika Huyo ambaye alikuwa na Msimu mzuri na timu ya Bidco kabla ya kujinga na timu ya Wazito,aliifungia Bidco mabao Sita.

Roland Ashimoto
Baada ya kujiunga na timu ya Wazito mwaka 2020, alijiunga na timu ya Kisumu All Stars kwa mkopo na baada ya mkopo kukamilika alirudi na kujiunga na timu ya Wazito Septemba mwaka jana .Baada ya kuvunja mkataba wake na timu ya Wazito amejiunga rasmi na timu ya Fc Talanta chini ya mkufunzi Ken Kenyatta.
Difenda Huyo mwenye miaka 20,alijiunga na timu ya Wazito kutokea Green Commandos ambayo ilikuwa chini ya Shule ya Upili ya wavulana ya Kakamega  .

Erickson Mulu Kivuva
Alijiunga na timu ya Wazito mapema Msimu huu kutoka timu ya Malaga City nchini Spain na kwa Mara anachezea timu ya Ligi Kuu.
Difenda Huyo alichezea timu ya Wazito kwa miezi Sita kabla Ya kuvunja mkataba wake .
Timu ya Wazito nchini ya mkufunzi mapya Fred Ambani baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Francis Kimanzi na benchi lake la ufundi kuondoka ,ameandikisha ushindi wa mechi mbili ,sare  moja na kupoteza mechi moja.