Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kenya yapoteza mechi mfululizo WAFCON

KENYA Pict

Muktasari:

  • Kenya ambayo ilianza kampeni kwa kuchapwa mabao 4-0 na wenyeji Morocco, imebakiza mechi moja dhidi ya Algeria huku ikiwa mkiani bila pointi.

NDOTO za timu ya taifa ya Kenya kufuzu robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026, zimefifia baada ya kupokea kichapo cha pili mfululizo katika Kundi A ikilala kwa bao 1-0 dhidi ya Senegal kwenye Uwanja wa Stade Olympique de Rabat, Morocco.

Bao pekee la mchezo lilifungwa na Seynabou Mbengue dakika ya 35, likiipa Senegal ushindi wa kwanza kwenye mashindano hayo na kufufua matumaini ya kusonga mbele. 

Kenya ambayo ilianza kampeni kwa kuchapwa mabao 4-0 na wenyeji Morocco, imebakiza mechi moja dhidi ya Algeria huku ikiwa mkiani bila pointi.


Licha ya matokeo hayo, mchezo ulikuwa wa ushindani mkubwa.

Kenya ilimiliki mpira kwa asilimia 51.4 dhidi ya 48.6 za Senegal, huku kila timu ikipiga mashuti sita yaliyolenga lango.

 Hata hivyo, Senegal ilionyesha umakini zaidi katika eneo la hatari na kutumia nafasi  moja muhimu kupitia Mbengue, tofauti na Kenya iliyoshindwa kuzitumia  ilizozipata.

Kwa mujibu wa takwimu za mchezo, Senegal ilipiga mashuti 21, Kenya 22, huku Senegal ikipata kona tano dhidi ya sita za Kenya. Kenya ilifanya makosa mara 18 dhidi ya 13 ya Senegal na kuonyeshwa kadi moja ya njano, wakati Senegal ilimaliza mchezo bila kadi yoyote.

Ushindi huo umeifanya Senegal kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Algeria kwa mabao 2-0. 

Kwa upande wa Kenya, ni kipigo cha pili mfululizo na sasa italazimika kuifunga Algeria katika mchezo wa mwisho huku ikitegemea matokeo ya timu nyingine ili ibaki na nafasi ya kusonga mbele.

Kenya inashiriki WAFCON kwa mara ya pili katika historia baada ya kurejea miaka 10 tangu ilipocheza kwa mara ya kwanza 2016. 

Katika ushiriki wake wa kwanza nchini Cameroon, Harambee Starlets ilimaliza mkiani mwa kundi baada ya kupoteza michezo yote mitatu ilichapwa kwa Ghana 3-1, Mali 3-1 na Nigeria 4-0, ikifunga mabao mawili na kuruhusu 10. Hivyo, hadi sasa bado haijawahi kushinda wala kutoka sare katika historia ya ushiriki wake WAFCON.